Dogo Janja na Irene Uwoya wamefunga ndoa kimya kimya - KULUNZI FIKRA

Sunday, 29 October 2017

Dogo Janja na Irene Uwoya wamefunga ndoa kimya kimya

 Muigizaji wa Filamu nchini Tanzania, Irene Uwoya jana Jumamosi amethibitisha kuwa amefunga ndoa, huku akiwaacha watu njia panda  kwa kutoweka wazi mwanaume aliyefunga nae ndoa.

Wikiendi hii Irene Uwoya kupitia ukurasa wake wa Instagram amekuwa bize kuposti picha zake akiwa ndani ya shela huku akimshukuru Mungu kwa kufanikisha zoezi hilo.

Licha ya Irene Uwoya kutomtaja mwanaume, marafiki zake wa karibu wamempongeza na kumtaja mwanaume huyo kuwa ni Dogo Janja.

Mtu wa kwanza kutoa pongezi kwa Irene Uwoya ni Mtangazaji wa Clouds TV, Zamaradi Mketema ambapo amemtaja Dogo Janja kwenye pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika “Hongera Sana kwa NDOA mpenzi wangu, mwanzo nilihisi ni movie lakini sasa nimeamini.. MUNGU awatangulie katika hili mlilolifanya @ireneuwoya8 @dogojanjatz kila la kheri INSHA’ALLAH!!”

Hata hivyo licha ya kuzagaa kwa taarifa hizo mitandaoni kuwa wawili hao wamefunga ndoa bado Dogo Janja hajatoa taarifa yoyote kuhusu tetesi hizo.

Watu wa karibu na Dogo Janja wamekanusha taarifa hizo lakini Madee kwenye mahojiano yake mafupi na kulunzifikra blog amethibitisha kuwa mwanaye Dogo Janja amefunga ndoa na harusi yake imefanyika Ijumaa ya wikiendi hii.

Madee pia akutaka kumtaja mwanamke aliyefunga ndoa na Dogo Janja, pia akuweza kuweka wazi mahali gani harusi ilifanyika.

No comments:

Post a Comment

Popular