Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kusitishwa mara moja kwa oparesheni ya kukamata mifugo katika pori tengefu la Loliondo na kuagiza mifugo iliyokamatwa kuachiwa mara moja.
Kigwangala amesema hayo leo na kusema mifugo mbalimbali ambayo imekamatwa na bado kufikisha mahakamani iachiwe bila masharti yoyote na wafugaji waendelea kutumia vyanzo vya maji ndani ya pori hilo.
Waziri Kigwangalla anasema maamuzi hayo aliyofanya ni hatua ambayo inalenga kutoa nafasi ya kushughulikia mgogoro huo kwa njia ya mazungumzo
Oktoba 19, 2017 Waziri Kigwangalla alitoa agizo kuwa mifugo na matrekta ambayo ipo kwenye pori Tengefu hilo la Loliondo viwe vimeondoshwa na kusema baada ya siku 7 mifugo na mali za watu hao vingekutwa kwenye pori hilo basi Serikali ingevitaifisha.

No comments:
Post a Comment