Aliyekuwa Waziri katika Serikali za awamu nne za kwanza, Stephen Wassira, amesema si jinai kuikosoa Serikali bali kuitukana ndiyo kosa kisheria.
Mwanasiasa huyo mkongwe nchini aliyewahi kuwa Mbunge wa Bunda kabla ya kushindwa na Esther Bulaya (Chadema) katika uchaguzi mkuu uliopita, ni miongoni mwa wanachama wa CCM waliojitokeza kuwania urais ndani ya chama hicho Uchaguzi Mkuu uliopita.
Akizungumza na kulunzifikra blog kwa njia ya simu jana akiwa nchini Marekani, Wassira ambaye alikuwa Waziri katika kipindi chote cha miaka 10 ya uongozi wa Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, alisema watu waikosoe Serikali kwa hoja na si kutukana.
"Ipo tofauti kati ya kutukana na kukosoa. Mimi naweza nikasema na bado nisitukane, mfano Zitto Kabwe (Mbunge wa Kigoma Mjini), huwa nasoma maandiko yake anaonekana ana hoja kabisa ambayo inahitaji kujibiwa na sijawahi kusikia akikamatwa.
"Lakini wapo wanasiasa; akisimama asipotukana hajisikii vizuri hao naona ndiyo wanaoshughulikiwa. Unaweza ukaikosoa Serikali bila kutukana, kukosoa Serikali si jinai lakini kutukana ndiyo jinai", alisema Wassira.
Kuhusu viongozi wa vyama vya siasa wanaokamatwa na vyombo vya dola pale wanapoikosoa Serikali, alisema hata kama wakikamatwa watakwenda mahakamani na baadaye mahakama itasema kama kuna kesi au laa.
"Akikamatwa si anakwenda mahakamani na kama hana kesi anaachiwa, hivyo pale mahakama inapotoa uamuzi kuwa hakuna kesi watapunguza ukamataji wa aina hiyo watawakamata wale wenye makosa tu", alisema.
Katika kushughulikia suala hilo, Wassira alilitaka jeshi la polisi kufanya kazi kwa uangalifu na kusisitiza kuwa watu wasiokuwa na hatia wasikamatwe.
"Jeshi la Polisi liwe na uangalifu, waendelee kufanya kazi lakini wasikamate watu wasio hatia", alisema Wassira.
Aidha, wanasiasa huyo mkongwe ambaye ameshiriki na kuongoza kamati maalumu iliyoandaa Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya mwaka 2015-2020, alizungumzia pia uongozi wa awamu zilizopita, akisema haiwezekani watu wote wawe na mtazamo sawa.
"Kuna siku niliulizwa swali kama hilo kuwa nimefanya kazi karibu na uongozi wote, nikaulizwa nani kafanana na nani na mimi nikasema hakuna anayefanana na mwingine.
"Nikimaanisha kwamba kila kiongozi ana style yake ya kuongoza. JK (Jakaya Kikwete) alikuwa anapenda kushirikisha watu wote anaopingana nao, alikuwa akiwakaribisha wapinzani wake lakini pamoja na yote hayo alitukanwa, aliitwa dhaifu.
"Amekuja JPM (Rais John Magufuli) wanasema ni mkali mara dikteta, lakini aliyekuwa mpole, msikilizaji wa maoni yao ni dhaifu. JPM anayesimamia misingi anayoiamini yeye wanasema ni dikteta... Kikwete aliwapa uhuru mwingi sana", alisema.
Akifafanua hoja hiyo, Wassira alisema Rais anayo haki ya kuongoza watu wake na pale wananchi wanapolalamika anao wajibu wa kuwasikiliza.
"Rais kama Kiongozi wetu ana wajibu wa kuwasikiliza wananchi wake na pale malalamiko yanapozidi lazima awasikilize na si lazima akakubaliana na kila kinachosemwa lakini ni wajibu wake kusikiliza.
"Kwa kusikiliza wanachokisema anaweza kupata ukweli na uongo... atatofautisha pumba na mchele na katika kuwasikiliza anaweza akaujua ukweli ambao alikuwa haufahamu", alisema Wassira.
Monday, 16 October 2017
Home
Unlabelled
Wassira: Kuikosoa serikali si jinai ni wajibu wa Rais kuwasikiliza wananchi wote
Wassira: Kuikosoa serikali si jinai ni wajibu wa Rais kuwasikiliza wananchi wote
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment