"Kuna majina ya watu wenye uwezo mkubwa sana sana ambao watatutoa hapa tulipo kama Jumuiya ila kwa kuwa Mwenyekiti ana watu wake mfukoni basi anakataa kabisa kuwapa nafasi na kuwapendekeza. Sisi tumeamua hatuwezi kuwa sehemu ya huu upuuzi, hivyo, tumeamua kutoka na tutafikisha malalamiko yetu na uhuni unaofanywa na Mwenyekiti katika vikao vya CHAMA" Moja wa mjumbe alisema.
Baada ya kushutumiwa, Mwenyekiti ndugu Sadifa alikasirika na kisha kuanza kuwapiga wajumbe wa Bara kwa chupa za maji walipokuwa wanatoka nje ya ukumbi Kitendo ambacho kilileta vuruga sana na mkutano kusimama kwa saa zima.
Hatimaye wajumbe wote kutoka Bara walitoka nje na kususia kikao hicho.


No comments:
Post a Comment