Wakandarasi wazawa waililia serikali katika upatikanaji wa tenda nchi - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 31 October 2017

Wakandarasi wazawa waililia serikali katika upatikanaji wa tenda nchi

 
 VYAMA vya wakandarasi vya Contractors Association of Tanzania, Tanzania Civic Engineering Contractors na Association of Citizen Contractors, wameiomba serikali iendelee kutoa fursa za kazi kwenye ujenzi wa miundombinu nchini.

Wakandarasi hao wameiomba serikali kupata kazi ya kujenga miundombinu kama reli, nishati, bomba la kusafirisha mafuta, ujenzi wa Makao Makuu ya Dodoma na sekta ya maji kwa wakandarasi wazawa.

Mwenyekiti wa Vyama vya Wakandarasi, Injinia Lawrence Mwakyambiki amesema hayo wakati akitambulisha siku ya wakandarasi ambayo itakayofanyika kila mwaka, kuwa wakipewa kazi hizo pesa watakazopata zitatumika kuinua uchumi ndani ya nchi.

“Wakandarasi wa hapa nchini wanaweza kukuza uchumi wa kwa sababu pesa wanazopata katika ujenzi zitasaidia kujenga hoteli au shule nchini kwetu,’’ amesema Injinia Mwakyambiki.

Injinia Mwakyambiki amesema lengo ya kuwa na siku ya wakandarasi ni kubadilishana uzoefu katika utendaji wa miradi mbalimbali na kutoa fursa kwa washiriki 200-300.
Aidha Injinia Mwakyambili amesema wanawashukuru wadau wa wakandarasi wakiwemo Commercial Bank of Afrika (CBA) na NMB Bank na wafadhili wengine kwa kuendelae kufanya kazi na wakandarasi wazawa.

Siku ya wakandarasi imepangwa kufanyika Novemba 17, mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Das es Salaam na itakuwa ikifanyika tarehe hiyo kila mwaka.

No comments:

Post a Comment

Popular