Familia ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu imesema kwamba kwa mara ya kwanza ndugu yao alipotolewa nje kupata hewa na kuota jua kauli yake aliyoitoa alisema kuwa ni sawa na ukiwa mfungwa huoni jua, mawingu wala hupigwi upepo wa kawaida.
Katika mahojiano aliyofanyiwa Kaka wa Lissu, Wakili Alute Mughwai Lissu amesema kwamba mara baada ya ndugu yake kutolewa nje na kukaa kwa takribani dakika 30 siyo yeye Lissu peke yake aliyefurahi bali ndugu wote waliokuwepo hospitalini hapo walifurahia mno hilo tukio.
Bw. Alute amesema kwamba awali Manesi walipanga kumtoa nje Jumamosi (Oktoba 14) na kwa kuwa Lissu alijua tunakwenda, aliwaeleza wasimtoe bali wasubiri ndugu zake wafike.
"Nilikuwa mimi na ndugu wengine. Ilipofika saa 10 jioni tulimtoa na mimi ndiye nilimtoa ICU, alifurahi na sisi tulifurahi kwa hatua hiyo,” amesema Kaka huyo mkubwa wa Lissu.
Alute ameeleza kwamba baada ya Lissu kupata upepo wa nje kwa nusu saa nzima alirudishwa wodini ambako amefafanua siyo ICU tena ingawa pia kuna ulinzi na uangalizi wa karibu na si kila mtu anaweza kumwona na kuongeza kwamba hali ya ndugu yake inazidi kuimarika huku akili zake zikiwa timamu.”
Pamoja na hayo Alute amesema kwamba suala la kumpeleka sehemu tofauti ya matibabu ndugu yao familia ndiyo itakayoshughulika zaidi kwa ukaribu na kuongeza kwamba, ndugu wengine wapo sehemu mbalimbali kama Kenya, Australia, Marekani, Canada ambao watabidi wajadiliane kwanza ndipo watatoa taarifa juu ya nini ya kinaendelea.
Wednesday, 18 October 2017
Home
Unlabelled
Tundu Lissu atoa ujumbe baada ya kutolewa nje kwa Mara ya kwanza
Tundu Lissu atoa ujumbe baada ya kutolewa nje kwa Mara ya kwanza
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment