Joshua Nassari: Siwezi kukaa kimya kama hatua hazitachukuliwa na Takukuru - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 18 October 2017

Joshua Nassari: Siwezi kukaa kimya kama hatua hazitachukuliwa na Takukuru

 Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA), Mhe Joshua Nassari amesema kuwa hatokaa kimya endapo haoni hatua zinazochukuliwa.

Nassari amesema hayo jana  Jumanne muda mchache baada ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Valentino Mlowola kumtaadharisha Nassari kuacha kugeuza taarifa anazoziwasilisha kwenye taasisi hiyo kuwa ni za kisasa.

Hata hivyo Nassari amesema, "Mlowola inabidi asome sheria ya "Whistle blower" ili nikae kimya lazima nione jitihada zinazofanyika kama hakuna nitaendelea kuongea.

"Sitokubali kutishwa ili nisiendelee kupeleka ushahidi ninachotaka kuona ni wahusika wanachukuliwa hatua sio madiwani, wahusika wakuu ni Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi".

Awali akizungumza jana Jumanne asubuhi, Mlowola ametoa tahadhari hiyo kwa Nassari leo Jumanne, Oktoba 17, 2017 alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

Amesema endapo Nassari ataendelea kuingiza siasa kwenye suala hilo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Mlowola amesema kitendo cha mwanasiasa huyo kuweka hadharani taarifa za uchunguzi ni kinyume cha sheria kwa kuwa kazi hiyo inatakiwa kufanyika kwa siri na mahakama ndiyo yenye jukumu la kuchukua hatua.

Amesema Takukuru ina wajibu wa kumlinda mtoa taarifa lakini jukumu hilo linakuwa tofauti kwa Nassari ambaye ameamua kujitokeza hadharani.

No comments:

Post a Comment

Popular