Siri yafichuka CCM juu ya mrithi wa katibu mkuu, Abdallah Bulembo kuwa mrithi wa Kinana - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 10 October 2017

Siri yafichuka CCM juu ya mrithi wa katibu mkuu, Abdallah Bulembo kuwa mrithi wa Kinana

 Ni Takribani wiki moja na siku kadhaa kumalizika kwa vikao vya juu vya chama cha Mapinduzi CCM mpaka sasa kumekuwa na minong'ono na mahojiano mbele ya wajumbe juu ya mstakabadhi wa nafasi ya ukatibu mkuu wa chama ambayo kwa sasa Ndg Abdulrahman Omar Kinana amejitabanaisha pasina shaka kuwa ahitaji kuendelea na nafasi hiyo hii ni kutokana na mambo kadhaa yalio tabanaishwa na baadhi ya wajumbe...

Mjumbe moja wa vikao vya juu vya CCM ambae hakupenda jina lake kufahamika ameilezea blog hii kuwa, Katibu mkuu kinana kwa sasa amesha peleka barua kwa mwenyekiti wa chama Taifa kujiondoa katika nafasi hiyo kwa kusema kwa sasa anamajukumu mengine na pia afya yake kwa sasa inamfanya kutoshiriki na kufanya majukumu yake vizuri,,

lakini undani wa swala hilo unaendana na mjumbe huyo kueleza kuwa " wanachama wa muda mrefu wa chama cha Mapinduzi wameshindwa kuelewa kwa sasa chama kinaendeshwa kwa faslafa ipi na ipi dira na malengo ya chama chao ikiwepo pia misingi ya kuanzishwa kwa chama hiki" alisikika mjumbe huyo ambae hakutaka jina lake lisemwe.

MRITHI WA KINANA.

Mjumbe huyo wa vikao vya juu vya chama cha mapinduzi ambae ameshika nafasi nyingi ndani ya serikali zikiwemo uwaziri na ukuu wa mikoa kadhaa na mwaka 2015 alikuwa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kuteuliwa na chama hicho kugombea na kukiwakilisha chama kwenye uchaguzi wa nafasi ya raisi wa Tanzania alienda mbali zaidi na kusema...

"Chama kwa sasa kimekosa dira na kufuata misingi ya kuanzishwa kwake kwa kuvunja miiko ya kimahusiano ilioachwa na waasisi wa taifa na chama chetu,, ndio maana leo nafasi ya ukatibu mkuu inaandaliwa kupewa raifiki wa karibu wa mwenyekiti wa chama"

Mjumbe huyo alienda mbali zaidi kwa kusema

"hakuwezi kukubali mtendaji mkuu wa chama kuwa Ndg. Abdallah Bulembo, kwanza hana historia iliotukuka ndani ya chama na mafanikio yasio tiliwa shaka na wanachama,, tumewaambia na tunaendelea kuwaambia,, wamemzuia asigombee nafasi ya mwenyekiti wa wazazi taifa ili wampe nafasi ya katibu mkuu wa chama kitu hicho kwetu kama wenye chama hatuko tayari kukiona kikitokea."

chanzo chetu kilipotaka kujua kwa ziada juu ya mpango unaoandaliwa wa Ndugu Abdallah bulembo kupewa nafasi ya kuwa katibu mkuu wa chama chanzo chetu cha taarifa "mjumbe wa vikao" alisema kwa sasa hawezi kulielezea kwa kina ila ndio lipo hivyo na wao wamejipanga kuhakikisha chama hakiendi kuangamizwa na watu wasiojua misingi ya chama.

Baada ya hapo chanzo cha taarifa hii kilitaka kufanya majukumu mengine na kuomba kwa sasa tumuacha afanye kazi nyingine,, mtandao huu ulitoa shukrani za dhati kwa mahojiano yaliofanyika kwa njia ya simu.

No comments:

Post a Comment

Popular