Rais Magufuli amkumbuka katibu wa zamani wa Bunge Kashilillah katika uteuzi wake - KULUNZI FIKRA

Friday, 27 October 2017

Rais Magufuli amkumbuka katibu wa zamani wa Bunge Kashilillah katika uteuzi wake

 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko katika safu ya Makatibu Wakuu, Naibu Makatibu Wakuu na Wakuu wa Mikoa kwa kuteua, kupandisha vyeo na kuhamisha vituo vya kazi.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi Ikulu Jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameteua na amewapandisha vyeo Naibu Makatibu Wakuu 4 na kuwa Makatibu Wakuu wapya na ameteua Naibu Makatibu Wakuu wapya 7 na amewahamisha vituo vya kazi Makatibu Wakuu 4 na Naibu Katibu Mkuu 1.
Aidha katika nafasi ya manaibu wapya waliopata nafasi ni pamoja na Aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanzania Thomas Kashillilah ambaye nafasi yake ilichukuliwa na Ndg. Stephen kigaigai, sasa amekuwa Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya Kilimo.

Aliyekuwa Katibu wa bunge kabla ya kung'olewa na kupewa tena nafasi ya kuwa Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya Kilimo Dkt homas Kashillilah
Orodha ya Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu ni kama ifuatavyo;
Ofisi ya Rais Ikulu.
Katibu Mkuu – Bw. Alphayo Kidata

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Katibu Mkuu (Utumishi) – Laurian Ndumbaro
Naibu Katibu Mkuu - Dorothy Mwaluko

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Katibu Mkuu - Mhandisi Mussa Iyombe
Naibu Katibu Mkuu(Afya) - Dkt. Zainabu Chaula
Naibu Katibu Mkuu(Elimu) - Bw. Tixon Nzunda
Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
Katibu Mkuu - Mhandisi Joseph Kizito Malongo
Naibu Katibu Mkuu - Bi. Butamo Kasuka Phillipo

Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Katibu Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) – Bw. Erick Shitindi
Katibu Mkuu(Bunge na Waziri Mkuu) - Maimuna Tarishi
Katibu Mkuu(Sera na Uratibu) - Prof. Faustine Kamuzora

Wizara ya Kilimo.
Katibu Mkuu - Mhandisi Methew Mtigumwe
Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Thomas Didimu Kashililah

Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Katibu Mkuu (Mifugo) - Dkt. Maria Mashingo
Katibu Mkuu (Uvuvi) - Dkt. Yohana Budeba

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Katibu Mkuu (Ujenzi) - Mhandisi Joseph Nyamuhanga
Katibu Mkuu (Uchukuzi) - Dkt. Leonard Chamriho
Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Dkt. Maria Sassabo
Naibu Katibu Mkuu (Mawasiliano) – Mhandisi Anjelina Madete

Wizara ya Fedha na Mipango.
Katibu Mkuu - Doto James Mgosha
Naibu Katibu Mkuu (Utawala) - Bi. Susana Mkapa
Naibu Katibu Mkuu (Fedha za Nje) – Bi. Amina Shaaban
Naibu Katibu Mkuu (Sera) - Dkt. Khatibu Kazungu

Wizara ya Nishati.
Katibu Mkuu - Dkt. Hamis Mwinyimvua

Wizara ya Madini.
Katibu Mkuu - Prof. Simon S. Msanjila

Wizara ya Katiba na Sheria.
Katibu Mkuu - Prof. Sifuni Mchome
Naibu Katibu Mkuu - Amon Mpanju

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Katibu Mkuu - Prof. Adolf F. Mkenda
Naibu Katibu Mkuu - Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
Katibu Mkuu - Dkt. Florence Turuka
Naibu Katibu Mkuu - Bi. Immaculate Peter Ngwale

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu - Meja Jen. Projest A. Rwegasira
Naibu Katibu Mkuu - Balozi Hassan Simba Yahaya

Wizara ya Maliasili na Utalii.
Katibu Mkuu - Meja Jen. Gaudence S. Milanzi
Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Aloyce K. Nzuki

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Katibu Mkuu - Dorothy Mwanyika
Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Moses M. Kusiluka

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Katibu Mkuu - Prof. Elisante Ole Gabriel
Naibu Katibu Mkuu (Viwanda) – Ludovick J. Nduhiye
Naibu Katibu Mkuu (Biashara na Uwekezaji) – Prof. Joseph Buchwaishaija

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Katibu Mkuu - Dkt. Leonard Akwilapo
Naibu Katibu Mkuu - Prof. James Epiphan Mdoe
Naibu Katibu Mkuu - Dkt. Ave-Maria Semakafu

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Katibu Mkuu (Afya) - Dkt. Mpoki Ulisubisya
Naibu Katibu Mkuu (Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto) - Bi. Sihaba Nkinga.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Katibu Mkuu - Bi. Suzan Paul Mlawi
Naibu Katibu Mkuu - Nicholaus B. William

Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Katibu Mkuu - Prof. Kitila Mkumbo
Naibu Katibu Mkuu - Mhandisi Emmanuel Kalobelo
 

No comments:

Post a Comment

Popular