Nyalandu: Tuendelee kummwombea Tundu Lissu, Nimeliona tabasamu la uso wake - KULUNZI FIKRA

Sunday, 15 October 2017

Nyalandu: Tuendelee kummwombea Tundu Lissu, Nimeliona tabasamu la uso wake

 
 Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), Mhe. Lazaro Nyalandu amesema kuwa ameliona tabasamu la uso wa Mbunge wa Singida Mashariki Mhe Tundu Antiphas Lissu na kusema kwamba Hakika Mungu anaendelea kujibu maombi ya watanzania.

"Tuendelea KUMWOMBEA ndugu yetu Tundu Lissu. Nimeliona TABASAMU la uso wake leo (Jana), na Hakika MUNGU anaendelea kujibu MAOMBI ya Watanzania wote wanaomkumbuka katika SALA na DUA zao katika MAJIRA na saa hii ya kujaribiwa kwake.

Tusimame PAMOJA naye, kwa kuwa SHAUKU ya MOYO wake ni kuiona siku iliyo njema, aweze kuifurahia kila ASUBUHI kama apendavyo MUNGU". Ameandika Mbunge huyo kwenye akaunti yake ya Facebook.

Picha ;

Lazaro Nyalandu na Kaka mkubwa wa Tundu Lissu, Advocate Lissu, Nairobi Hospital mapema jana.

No comments:

Post a Comment

Popular