Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) amewasilisha ushahidi mwingine kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu tuhuma za ununuzi wa madiwani wa Chama hicho.
Madiwani hao nane wa Chadema wamejiuzulu kwa kile walichoeleza kumuunga mkono Rais John Magufuli jambo ambalo Nassari anadai siyo kweli bali walinunuliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo nje ya ofisi ya Takukuru Upanga jiji ni humo amesema, " huu ni ushahidi wa tatu na kadri upepelezi ukiwa unaendelea nitaleta mwingine, hii ni kama filamu ya Isidingo."
Nassari amesema alitarajia Rais John Magufuli angewachukulia hatua wateule wake wanaohusishwa katika sakata hilo ili kupisha uchunguzi uweze kufanyika kwa uhuru.
"Tunajiuliza kwa nini Rais hawachukulii hatua DED, DAS au DC wote wa Arumeru kwa kutuhumiwa, watupeleke mahakamani na tungeomba suala hili lichukuliwe kwa uzito wake," amesema Nassari
Naye Mbunge wa Ubungo, Saed Kubunea aliyeongozana na Nassari amesema,"Mimi nimeshiriki hususani kihabari kwani nimewashauri hawa kuutoa kwa umma ili jamii ijue ukweli."
"Tunachojiuliza kwa nini rais yupo kimya, kwa nini mawaziri na viongozi waliotuhumiwa Katika sakata la Almas na Tanzanite aliwasimamisha kwa nini hawa hataki," amehoji Kubenea
Monday, 16 October 2017
Home
Unlabelled
Nassari akabidhi ushahidi mwingine Takukuru
Nassari akabidhi ushahidi mwingine Takukuru
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment