Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kesho Jumanne Oktoba 17, 2017 atazungumzia maendeleo ya afya ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Lissu aliyeshambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akiwa katika makazi yake Area D mjini Dodoma Septemba 7, amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea na matibabu.
Akizungumza na kulunzifikra blog leo Jumatatu, baada ya kuulizwa kuhusu hali ya Lissu, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema:
“Kesho saa 5:00 asubuhi nitakuwa na mkutano na waandishi wa habari, nitazungumzia hali ya Lissu na mambo mengine yanayoendelea.”
Baadaye katika taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha chama hicho, Tumaini Makene amesema mkutano huo utafanyika makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam.
“Kupitia Mwenyekiti, Freeman Mbowe chama kitatoa taarifa kwa Taifa kuhusu maendeleo ya Tundu Lissu, mrejesho wa michango, gharama za matibabu,” amesema Makene
Monday, 16 October 2017
Home
Unlabelled
Freeman Mbowe kuelezea maendeleo ya afya ya Tundu Lissu kesho
Freeman Mbowe kuelezea maendeleo ya afya ya Tundu Lissu kesho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment