Akizungumza Jana Jumamosi katika mkutano na waandishi wa habari Gambo amesema wanaosambaza uvumi kuwa atagombea ubunge Arusha ni wanasiasa ambao hawajiamini na wameshindwa kutatua kero za wananchi.
"Kazi ambazo nafanya kwa kushirikiana na wasaidizi wangu wakuu wa wilaya ni kutatua kero na tumeachana na mambo ya kisiasa kutembea na flashi wafanye wao sisi tunachapa kazi," amesema Mrisho Gambo.
Amesema ni ukweli uliowazi baadhi wabunge hawaonekani majimboni na hivyo kuwaachia viongozi wa Serikali kufanya kazi ambazo zilipaswa kufanywa na wabunge.
Akizungumzia tuhuma za kununuliwa madiwani wa Chadema ambazo zilitolewa na wabunge wa Chadema, Joshua Nassari na Godbless Lema, Gambo amesema anaamini hakuna masuala ya rushwa.
Gambo amesema madiwani ambao wamejiuzulu wameridhishwa na utendaji kazi mzuri wa Rais Magufuli.
"Kuna madiwani wameondoka Arusha, Monduli, Ngorongoro, Arumeru, Hai, Iringa na maeneo mengine hawa wote wameridhishwa na utendaji wa Serikali ya awamu ya tano," amesema Mrisho Gambo.
Saturday, 14 October 2017
Home
Unlabelled
Mrisho Gambo: Sina mpango wa kugombea ubunge jimbo la Arusha mjini
Mrisho Gambo: Sina mpango wa kugombea ubunge jimbo la Arusha mjini
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment