Dar es salaam: Sheikh Ponda aachiwa na jeshi la polisi kwa dhamana - KULUNZI FIKRA

Saturday, 14 October 2017

Dar es salaam: Sheikh Ponda aachiwa na jeshi la polisi kwa dhamana

 
 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemwachia kwa dhamana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.

Pondà ameachiwa Jana  Jumamosi jioni baada ya kushikiliwa na Jeshi hilo tangu jana Ijumaa asubuni akituhimiwa kutoa lugha za kichochezi katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatano iliyopita.

Akizungumza na kulunzifikra blog  Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimba amesema: "Sheikh Ponda ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kuripoti tena polisi."

Awali, Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa aliambia kulunzifikra blog kwamba uchunguzi dhidi ya Ponda ulikuwa ukiendelea na kama ungekamilika angepewa dhamana.

"Upelelezi unaendelea na ukikamilika tutaangalia kama atapata dhamana au tutampeleka mahakamani," alisema Mambosasa kabla ya Sheikh Ponda kuachiwa.

Wakili wa Ponda, Profesa Abdallah Safari amesena: "Ni kweli Sheikh Pondà ameachiwa, ni lini atarudi tena sijajua ila sidhani kama watampeleka mahakamani."

No comments:

Post a Comment

Popular