Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tunduma, Herode Jivava ametiwa nguvuni na Polisi akidaiwa kutishia kuua kwa maneno.
Jivava ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Songwe anakuwa kiongozi wa nane kukamatwa na kuwekwa mahabusu. Baadhi ya waliokamatwa wamefunguliwa kesi mahakamani na wengine wako nje kwa dhamana wakisubiri upelelezi wa polisi kukamilika.
Akizungumza kuhusu kukamatwa kwa Jivava, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa Songwe, Ayub Sikagonamo amesema alikamatwa jana Jumapili jioni mjini Vwawa akijiandaa kuingia uwanjani kuangalia mpira na alipelekwa Kituo cha Polisi Tunduma.
“Asubuhi hii tumefika hapa Polisi tumeambiwa Jivava anatuhumiwa kwa kosa la kutishia kuua kwa maneno. Eti aliwatishia mgambo wakati wakiwaondoa kwa nguvu Machinga mjini Tunduma,” amesema.
Sikagonamo amesema wanamsubiri mwanasheria ili kushughulikia suala hilo. Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange hakuwa tayari kuzungumzia taarifa za kukamatwa kwa Jivava.
Tuesday, 10 October 2017
Home
Unlabelled
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Tunduma (Chadema) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kutishia kuua kwa maneno
Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Tunduma (Chadema) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kutishia kuua kwa maneno
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment