Lazaro Nyarandu mbunge wa Singida Kwa tiketi ya CCM, ameiacha CCM kimya kimya na kinachosubiriwa ni kutangaza rasmi kuhamia Chadema, imebainika.
Taarifa toka Singida na Jimboni kwake zinabainisha kwamba mbunge huyo amesitisha kabisa kushiriki vikao vya CCM na kujihusisha na masuala yote ya kichama na badala yake yuko bize Kwenda Nairobi kufanya mazungumzo na Viongozi wa upinzani.
Taarifa za uhakika toka Singida zinamtaja Mbunge huyo kusitisha mahusiano na chama chake na hahudhurii vikao muhimu ndani ya wilaya yake hasa vikao vya kamati ya siasa ya wilaya Kwa muda wa miaka 2 sasa hajahudhuria kikao cha kamati ya siasa na Halmashauri kuu ya CCM wilaya. Vikao hivi ni muhimu sana katika kutoa dira ya uongozi wa kisiasa na masuala ya Maendeleo.
Mfano katika uchaguzi Mkuu wa CCM 2017 ngazi ya wilaya. Nyarandu anatajwa kugoma kutoa ushirikiano Kwa CCM Singida kaskazini katika mchakato wa uchaguzi ndani ya eneo lake la wilaya. Haikuishia hapo, wakati CCM Singida kaskazini Wameitisha Mkutano mkuu wa CCM wilaya Kwa ajili ya kuwachagua Viongozi wa wilaya mnamo October 5,2017 Mbunge huyo hakuhudhuria Mkutano huo muhimu ndani ya wilaya yake na badala yake alionekana Mkoani Mwanza Kwenye makongamano ya kidini akihubiri madhabahuni. Kitendo chá Mbunge kukataa kuhudhuria Mkutano wa uchaguzi muhimu ndani ya wilaya yake kinathibitisha ukweli kwamba kiongozi huyo ameitoa CCM ndani ya moyo wake.
Katika uchaguzi Mkuu wa CCM Singida kaskazini maswahiba wa karibu sana wa Nyarandu wanatajwa kupigwa chini na kupoteza nafasi zao za uongozi ndani ya chama hicho, akiwemo mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo ambae ndiyo pumzi ya Nyarandu Kwa zaidi ya miaka 20, na Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo ambae ni swahiba mkubwa wa Nyarandu amepoteza uongozi ndani ya chama hicho kupitia uchaguzi wa mwaka huu.
Ndani ya Mkutano mkuu wa CCM Singida kaskazini inatajwa wana CCM walikuwa wakipashana Habari kuhusu mbunge wao Kuwa na mpango Kwenda upinzani ndiyo maana amekataa kuhudhuria Mkutano huo muhimu ndani ya wilaya yake. Watu wake wa karibu waliogombea walisulubiwa Kwenye kura kutokana na Matendo ya mbunge huyo kutowajibika Kwa wananchi na Mienendo yake isiyoeleweka.
Watu wake wa karibu waliogombea na kushindwa Kwenye uchaguzi wamenukuliwa wakisema watahamia upinzani Kwa muda mwafaka. Kauli hizi Kwa watu wa karibu mno na mbunge huyo zinaleta picha kamili wanachopanga na watu wake, Kinachoendelea Kwa sasa ni kukamilisha mipango hiyo hatua Kwa hatua. Matendo ya Kiongozi huyo Kwa sasa yanaashiria uhalisia huo.
Jambo muhimu ambalo wengi hawajui ni kwamba Nyarandu ni mtiifu Kwa Edward Lowassa Kwa muda mrefu sana na ni mtu wake wa karibu, hapo katikati uhusiano wao Ulikuwa Kwa usiri hasa kuelekea uchaguzi Mkuu wa 2015 ambapo Lazaro naye alikuwa ni mgombea urais kupitia CCM. Uhusiano wake na Lowassa Kwa sasa umeimarika maradufu na wamekutana mara kadhaa Kwenye moja ya hotel mkoani Arusha
Friday, 20 October 2017
Home
Unlabelled
Lazaro Nyalandu aiacha ccm kimya kimya
Lazaro Nyalandu aiacha ccm kimya kimya
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
Hata wao wanaona mwelekeo na aman Vietoweka ndan ya chama
ReplyDelete