Wakati mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu akielezea kuwa anakusudia kuwasilisha hoja ya muswada binafsi kwa spika utakaoweka sharti la kurejea upya mjadala wa katiba mpya, utafiti umeonyesha kuwa wananchi wawili kati ya watatu wanasema Tanzania inahitaji katiba mpya.
Pia, nusu ya wananchi wamesema mchakato wa katiba mpya uanze upya na tume mpya.
Jana katika akaunti zake za mitandao ya kijamii ya Instagram, Twitter na Facebook Nyalandu aliandika.
"Nakusudia kuwasilisha kwa spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai azma yangu ya kuleta muswada binafsi wa sheria katika kikao kijacho cha Bunge itakayoweka sharti la kurejea upya mjadala wa katiba mpya ya Tanzania kwa kuzingatia rasmu ya katiba iliyowasilishwa na tume ya jaji Warioba", aliandika Nyalandu.
Nyalandu alisema muswada huo anatarajia kuwasilisha kwenye kikao kijacho cha Bunge.
Akizungumza na kulunzifikra blog kwa njia ya simu baada ya kuandika maneno hayo, Nyalandu alisema amekusudia kupeleka muswada huo kwa sababu mchakato wa katiba mpya haukufikia mwisho.
"Nitafurahi sana kama jambo hili litafanikiwa kwa kuwa Luna umuhimu wake kwa kila mtu. Suala hili pia halima Itikadi za vyama vya siasa na lina masilahi kwa taifa, kwa sababu katiba INA uwezi wa kukaa zaidi ya miaka 100", alisema Nyalandu.
No comments:
Post a Comment