Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA) Joshua Nassari amefunguka na kusema maisha yake yapo hatarini na kudai kuwa watu ambao amewaanika kwenye sakata la ununuzi wa madiwani wanamtafuta.
Nassari amesema hayo ikiwa imepita siku moja toka alipokwenda kwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kupeleka ushahidi wake juu ya madiwani wa CHADEMA waliohama chama kwa kuhongwa rushwa na wateule wa Rais John Pombe Magufuli.
"Maisha yangu yapo kwenye bonde la uvuli wa mauti, Maisha yangu yapo hatarini kwani Watesi wetu wananitafuta" aliandika Nassari kupitia ukurasa wake wa facebook.
Mbali na hilo wachangiaji mbalimbali kwenye ukurasa wa Mbunge huyo walimtaka azidi kumuomba Mungu huku wakimshauri kuongeza ulinzi zaidi katika maisha yake ya kila siku kutokana na jambo ambalo ameliibua na kumtaka aendelee kupambana, baadhi ya wachangiaji wengine wamedai kuwa anachofanya ni njia ya kujitafutia umaarufu kisiasa.
Juzi Mbunge Joshua Nassari, Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa walikwenda kwenye Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kupeleka ushahidi wao juu ya sakata la kununuliwa kwa madiwani wa CHADEMA na kuhongwa fedha na ahadi mbalimbali kutoka kwa wateule wa Rais mkoani Arusha.
Tuesday, 3 October 2017
Home
Unlabelled
Joshua Nssari: Maisha yangu hapo hatarini wabaya wangu wananiwinda kila kona
Joshua Nssari: Maisha yangu hapo hatarini wabaya wangu wananiwinda kila kona
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment