Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ambaye ndiye mwenye mamlaka ya kuizungumzia afya ya Mbunge, Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana, amesema hali ya mwanasiasa huyo inaendelea vizuri huko nchini Kenya anapopatiwa matibabu.
Akizungumza na kitengo cha habari cha chama hicho, Mbowe amelitaka jeshi la polisi nchini kuongeza kasi ya upelelezi huku akidai dereva ambaye alikuwa anamuendesha Mbunge huyo wa Singida anaendelea na matibabu ya kisaikolojia ambapo pia amedai wanaogopa kumrudisha nchini Tanzania kutokana na hali ya usalama.
“Kwa sababu leo ni siku 32 zimepita jeshi la polisi linasema linamsubiri dereva wa Lissu lifanye uchunguzi, dereva wa Lissu tupo naye Nairobi anaendelea kupatiwa matibabu ya kisaikolojia kwa sababu aliona tukio lakutisha na vile vile kumrejesha Tanzania katika hali ambayo hatujapewa uhakika wa usalama wake, wanaweza bado wakamuua, wakamtoa roho yake, ndio maana tukasema lazima tumlinde kama tunavyomlinda Mhe Lissu kule hospitali analindwa na maaskari wenye bunduki,” alisema Mbowe
Monday, 9 October 2017
Home
Unlabelled
Freeman Mbowe: Dereva wa Tundu Lissu akirudi Tanzania anaweza akauawa
Freeman Mbowe: Dereva wa Tundu Lissu akirudi Tanzania anaweza akauawa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment