Arusha: Wakili wa anayemtetea Lema ajitoa kwenye kesi ya Lema baada ya Hakimu kukutaa kujitoa - KULUNZI FIKRA

Monday, 9 October 2017

Arusha: Wakili wa anayemtetea Lema ajitoa kwenye kesi ya Lema baada ya Hakimu kukutaa kujitoa


Wakili Sheck Mfinanga, anayemtetea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema katika kesi ya uchochezi amejitoa katika kesi hiyo kwa madai kuwa haridhishwi na mwenendo wa shauri hilo ikiwamo hakimu kugoma kujitoa. Lema aomba muda kutafuta Wakili mwingine au kujitetea mwenyewe

Mbunge wa Arusha mjini Leo akitoka na mafaili ya kesi mahakama ya wilaya ya Arusha baada ya wakili wake kujitoa
Wakili wa mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, Sheki Mfinanga amejitoa kuendelea kumwalisha mbunge huyo baada ya kutoridhishwa na namna shauri hilo linavyoendeshwa.

Septemba 25, mwaka huu alimuomba hakimu anayesikiliza shauri hilo la jinai namba 440/2016 Kaimu Hakimu mkazi Mfawidhi, Desder Kamugisha ajitoe kuendelea na shauri hilo kwani mteja wake hana imani naye lakini hakimu huyo aligoma huku akitumia vipengele vya sheria vinavyompa nguvu hiyo.

Sheki aliwasilisha kusudio na mdomo la kukata rufaa mahakama Kuu hivyo akaomba mwenendo wa shauri hilo usimame ili waweze kukamilisha taratibu za kupeleka rufaa yao.

Hata hivyo hakimu Kamugisha alikataa ombi hilo la kusimamisha mwenendo na kuagiza upande wa Jamhuri ulete mashahidi wao leo kwa ajili ya kuendelea.

"Mheshimiwa hakimu nilitoa ombi la mdomo kupatiwa nakala ya mwenendo wa kesi septemba 25, sikupatiwa nikakumbushia kwa barua oktoba 2 na Leo asubuhi nimewasilisha barua nyingine ya kukumbushia lakini mpaka Sasa sijapatiwa," amesema Mfinanga mahakamani hapo.

lema.jpg

No comments:

Post a Comment

Popular