Chama cha Wananchi (CUF) upande wa Katibu Mkuu, Maalim Seif kimefunguka na kusema kitashirikiana na UKAWA katika uchaguzi mdogo ambao unatarajia kufanyika hivi karibuni, CUF kimezitosa hoja za Lipumba ambao walisema hawezi kushirikiana na UKAWA.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Mbarala Maharagande amesema hayo leo na kudai tayari wao wameanza mashirikiano baina ya vyama vinavyounda UKAWA na kuwa tayari wameshapeana majukumu ya kutekeleza mpaka Oktoba 23, 2017 ambapo watakutana na kufanya marejesho ya hatua walizofikia katika kufanya mgawanyo wa Kata mbalimbali ili kuunganisha nguvu ya upinzani katika uchaguzi.
Aidha Mbarala amesema kuwa wao kama CUF msimamo wao ni kushirikiana na wagombea wa vyama vingine katika Kata hizo na kufanya kampeni za bega kwa bega ili kuhakikisha ushindi unapatikana.
"Uchaguzi ni Mkakati. Viongozi na Vyama makini hawawezi kwenda katika uchaguzi bila ya kuzingatia hayo na kufanya Uchambuzi wa kutosha wa taarifa na Takwimu (Comprehesive Data, Facts and Information Analysis/ Environmental Scanning). Viongozi wa ngazi ya Taifa watatoa tamko la pamoja kwa wakati muafaka kuonyesha mgombea wa chama kipi anayepeswa kuungwa mkono katika Kata husika. Niwajibu wetu kuthibiti hujuma mbalimbali zinazoweza kufanywa na CCM, Tume (Maafisa uchaguzi) na vibaraka wao" alisema Mbarala
Mbali na hilo taarifa hiyo ya CUF imesema kuwa chama hicho hakikuundwa kwa lengo la kukisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kutawala Watanzania
Oktoba 7, 2017 Chama cha CUF upande wa Prof. Ibrahim Lipumba, kilisema kuwa hakitashirikiana na umoja wa vyama vya upinzani nchini (UKAWA) na hawana mpango wa kushirikiana nao kwenye uchaguzi ujao.
Friday, 13 October 2017
Home
Unlabelled
Cuf ya upande wa Maalim Seif wamtosa Prof Lipumba, wasema watashirikiana na ukawa katika uchaguzi mdogo
Cuf ya upande wa Maalim Seif wamtosa Prof Lipumba, wasema watashirikiana na ukawa katika uchaguzi mdogo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment