CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini ( IGP), Simon Sirro kuacha kutoa vitisho kwa wananchi na wanasiasa kwa kuwataka waache kuzungumzia tukio la Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), (Tundu Lissu kupigwa risasi 38 mkoani Dodoma kwa kuwa hiyo siyo kazi yake.
Chadema wamesema hakuna sheria yoyote inayompa Sirro mamlaka hayo na kwamba anatakiwa kuacha kutoa kauli za kuwanyamazisha.
Kauli hiyo ya Chadema, imetolewa Jana na Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya alipozungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho.
Amesema Sirro hana ubavu wa kuzuia watu wakiwamo wanasiasa kuendelea kujadili suala hilo.
“Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki na fursa kwa wananchi kutoa maoni na mawazo yao na kupashana habari pamoja na sheria nyingine na ibara hii ndio msingi, ” amesema Malya.
Aidha, ameeleza kuwa Sirro anaongozwa na sheria kubwa ya jeshi la polisi na huduma saidizi ambayo inatoa maelezo ya nani anaweza kumuamuru, na kuwa na mamlaka ya kuamuru askari wake na siyo raia wa kawaida.
“IGP anyamaze andelee na upelelezi, msisikilize Sirro anachoeleza hamvunji sheria kwa kujadili nani amejaribu kumuua Tundu Lissu, msiingilie upelelezi wao sawa, msiwazuie kufanya upelelezi sawa lakini jadilini,” amesema.
Wednesday, 11 October 2017
Home
Unlabelled
Chadema wamtaka IGP Sirro kuacha vitisho kuhusu sakata la Tundu Lissu
Chadema wamtaka IGP Sirro kuacha vitisho kuhusu sakata la Tundu Lissu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...

No comments:
Post a Comment