Zitto kabwe atoa maneno mazito kwa spika Ndugai - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 12 September 2017

Zitto kabwe atoa maneno mazito kwa spika Ndugai

 Kwa kutumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter Mheshimiwa Zitto Kabwe amesema haya juu ya Spika wa Bunge Mheshimiwa Ndugai

 "Spika Ndugai anajua ninavyomheshimu. Kama imefikia haoni heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia. Nitakwenda Kamati ya Maadili"

"Spika Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya Nchi yetu kushuhudia Mbunge anapigwa risasi Mkutano wa Bunge ukiendelea"

"Wabunge wazoefu tulikuwa na matumaini makubwa na Spika Ndugai, tulimpigania dhidi ya njama za kumhujumu kutoka Ikulu. Anatuangusha"

    Mheshimiwa Zitto, anaendelea kusema kuwa

"Spika Ndugai, angejua nguvu aliyonayo kukabili udikteta unaonyemelea nchi yetu asingehangaika na ukosoaji wenye staha tunaoufanya"

"Kwenye mazishi ya Spika wa Watu Mzee Sitta, Ndugai aliomba afike japo robo ya Sitta. Hajafika hata 10% ya Anna Makinda miaka 2 Sasa"

"Hatujawahi kuwa na Spika anayedhalilishwa Na Rais Kwamba aliuliza wajumbe gani awaweke Kamati za uchunguzi za Bunge"
    

No comments:

Post a Comment

Popular