Zitto kabwe akamatwa na polisi uwanja wa Ndege Dar - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 20 September 2017

Zitto kabwe akamatwa na polisi uwanja wa Ndege Dar

 Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT –Wazalendo), Zitto Kabwe amekamatwa na polisi akiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) akitokea Kigoma.

Ofisa Habari wa ACT-Wazalendo, Abdallah Khamis amesema Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa chama hicho amekamatwa jioni hii.

Jana Jumatano asubuhi, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema Zitto atafutwe, akamatwe na kufikishwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.

Alisema Zitto alipewa barua ya wito wa kufika mbele ya kamati hiyo baada ya Spika Job Ndugai kuagiza hilo lifanyike lakini hajalitekeleza.

No comments:

Post a Comment

Popular