Kupona kwa Mhe. Lissu ni mpango wa Mungu, nawaomba Watanzania wenzetu waendelee kumuombea kwa Mungu pamoja na kuchangia gharama za matibabu, kwa kuwa gharama zake ni kubwa ambazo chama pekee hakiwezi kuzimudu bila ya misaada kutoka kwa watu mbalimbali.
Unajua ahueni humtokea mgonjwa taratibu taratibu na ndivyo inavyotokea kwa Lissu, ingawa sisi wote tuna hamu apone mara moja aje aendelee kupigania haki za wanyonge kama alivyokuwa akifanya.
Sisi tunatoa taarifa za maendeleo ya Lissu kulingana na Madaktari wanavyotuambia, hatuwezi kusema chochote nje ya wataalam hao, kwa kuwa ndio wenye ujuzi wa kumtibu na kujua maendeleo ya mgonjwa husika.
UPINZANI NI KAZI NGUMU Kazi ya Upinzani ni ngumu, hasa katika zama za utawala wa awamu ya tano, ambae inaonekana hatambui na kuthamini mchango wa Wapinzani kama walivyokuwa watangulizi wake.
Licha ya vitisho na kila aina ya hujuma tunazofanyiwa kamwe hatuwezi kurejea nyuma, bali tutafanya kazi zetu kwa tahadhari kubwa kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma ambapo tulikuwa na Uhuru mkubwa wa kujieleza na Serikali kufanyia kazi mambo tunayosema.
Huwezi kuendesha nchi bila kuruhusu ukosoaji, iwe kutoka upinzani au kwenye chama unachokiongoza, unapowazuia watu wasipumue na kutoa madukuduku yao, unatengeneza hasira kubwa ndani ya jamii.
Thursday, 21 September 2017
Home
Unlabelled
Freeman Mbowe: Kupona kwa Mhe Lissu ni mpango wa Mungu, watanzania tuendelee kumuombea
Freeman Mbowe: Kupona kwa Mhe Lissu ni mpango wa Mungu, watanzania tuendelee kumuombea
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment