Serikali yatoa tamko matibabu ya Lissu - KULUNZI FIKRA

Thursday, 21 September 2017

Serikali yatoa tamko matibabu ya Lissu

 Serikali imesema ipo tayari kugharamia gahrama za matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu katika hospitali yoyote duniani, iwapo familia itaomba jambo hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu , na kusema kwamba kama familia itahitaji na ripoti ya madaktari ikionyesha kuna ulazima, serikali itasimamia suala hilo.

Hivi karibuni kumekuwa kukiendeshwa kampeni ya kuchangia matibabu ya Tundu Lissu baada ya gharama zake za matibabu kuwa kubwa huku watu wakiitupia lawama serikali.

No comments:

Post a Comment

Popular