James Kotei atoa ujumbe mzito kwa mashabiki wa Simba - KULUNZI FIKRA

Thursday, 21 September 2017

James Kotei atoa ujumbe mzito kwa mashabiki wa Simba

 SIMBA inarejea uwanjani leo Alhamisi kusaka usukani wa Ligi Kuu Bara ugenini dhidi ya Mbao FC, huku rekodi zikionyesha hakuna nam bibna ya kuwazuia tena.

Washindi hao wa Kombe la FA kwanza hawajawahi kupata hata sare dhidi ya Mbao katika mechi tatu walizokutana kwani wameshinda zote. Rekodi nzuri zaidi ni kwamba waliifunga Mbao mabao saba katika mechi hizo tatu huku wao wakiruhusu matatu tu.

Mtanange huo unapigwa siku 114 tu tangu walipokutana kwenye mechi ya fainali ya Kombe la FA ambapo Simba ilishinda 2-1 katika mchezo huo uliokwenda dakika 120.

Mchezaji Bora wa fainali hiyo ya FA, James Kotei, ambaye ndiye aliyemilikishwa namba ya Jonas Mkude, anasema kwa sasa hakuna namna ya kuwazuia Simba kwani wako moto kinoma.

“Tuko moto kwa sasa, ni ngumu kwa timu yoyote kutuzuia,” alisema Kotei aliye chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Joseph Omog.

“Tunaifahamu Mbao ni timu yenye ushindani mkubwa, lakini haiwezi kutuzuia sasa, tunachowaza sisi ni ushindi tu.”

OKWI AIBU

Wakati Simba ikiwa tayari kushuka uwanjani leo, habari kubwa ni straika wake, Emmanuel Okwi, ambaye amefunga mabao sita katika mechi mbili msimu huu.

Okwi kwa sasa anashikilia rekodi ya kufunga bao kila baada ya dakika 30 uwanjani akiwapiku kwa mbali washambuliaji wengine kama Ibrahim Ajibu wa Yanga aliyefunga bao moja kwa dakika 270 alizocheza.

Okwi pia amefunga mabao mengi sawa na yale ya Yanga, Azam, Stand United, Kagera Sugar na Ndanda kwa pamoja.

Timu hizo zote kwa ujumla wake zimefunga mabao sita tu msimu huu.

Mshambuliaji huyo anayeichezea pia timu ya Taifa ya Uganda, ametumia mechi mbili tu kufunga nusu ya mabao yake ya msimu wa 2011/12 ambapo kwa msimu mzima alifunga mara 12.

No comments:

Post a Comment

Popular