NAMBA hazidanganyi bwana. Hakuna shabiki yeyote wa soka kwa sasa anayehoji tena ubora wa Emmanuel Okwi. Hata waliokuwa wakimuita Mhenga sasa wamenyamaza baada ya Mganda huyo kuwanyamazisha mashabiki hao.
Dakika 180 alizotumia katika mechi mbili kati ya tatu ambazo timu yake imecheza imethibitisha kuwa Okwi sio mtu wa mchezomchezo.
Mganda huyo alitupia kambani mabao mawili safi wakati Simba ikichapa Mwadui mabao 3-0 na kumfanya kufikisha mabao sita. Manne aliyafunga katika mechi ya ufunguzi dhidi ya Ruvu Shooting, Simba iliposhinda mabao 7-0.
Mabao sita ya Okwi ni mara mbili ya yale yaliyofungwa na kikosi kizima cha Yanga chenye mabao matatu tu katika mechi tatu.
Kama haitoshi ukiyachanganya mabao ya Yanga na mawili ya Azam, bado hayafikii idadi ya magoli yaliyofungwa na Okwi.
Tuesday, 19 September 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment