Tume ya Umoja wa Mataifa-UN nchini Congo inasema mlinda amani mmoja ameuwawa kufuatia mapigano katika eneo la Beni kwenye jimbo la Kivu kaskazini nchini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press-AP tume hiyo ilisema Jumatatu kwamba mlinda amani huyo raia wa Tanzania alipigwa risasi wakati wa shambulizi la Jumapili lililofanywa na washukiwa waasi wa kundi la Allied Democratic Forces kwenye eneo la vikosi vya jeshi.
Ilisema eneo la jeshi lilikuwa kiasi cha mita 500 kutoka kwenye kituo cha Umoja wa Mataifa. Tume ya Umoja wa Umoja ilisema mlinda amani mwingine raia wa Tanzania alijeruhiwa katika mapigano na amehamishiwa kwenye hospitali ya Umoja wa Mataifa huko Goma.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres alilaani mauaji hayo na aliisihi serikali ya Congo kuchunguza tukio hilo na kuwafikisha waliohusika mbele ya sharia. Katika taarifa yake aliyataka makundi yote yenye silaha nchini Congo kusitisha ghasia
Tuesday, 19 September 2017
Home
Unlabelled
Mlinda amani wa UN raia wa Tanzania wameuawa nchini Congo na mwingine ajeruhiwa
Mlinda amani wa UN raia wa Tanzania wameuawa nchini Congo na mwingine ajeruhiwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment