Rais John Magufuli leo Jumatano anatarajiwa kutua Arusha kwa ziara maalumu ambapo mapema asubuhi atafungua barabara ya Kami kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia) hadi Mererani wilayani Simanjiro.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema Rais Magufuli anatarajiwa kupokewa uwanja wa ndege wa Kilimanjaro saa mbili asubuhi.
Gambo amesema baada ya kupokelewa atakwenda Mererani Mkoa wa Manyara kuzindua barabara ya Kia-Mererani yenye urefu wa kilomita 26.
Amesema baada ya uzinduzi huo atazungumza na wananchi na baadaye kurejea Arusha. Gambo amesema Rais Magufuli anatarajiwa kutoa kamisheni kwa maafisa waliohitimu mafunzo ya jeshi katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jumamosi.
"Napenda kutumia fursa kuwaomba wakazi wa Arusha kujitokeza Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Septemba 23 kuanzia saa 12:30 asubuhi,"amesema.
Wednesday, 20 September 2017
Home
Unlabelled
Rais Magufuli ziarani Arusha leo
Rais Magufuli ziarani Arusha leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment