Straika wa Simba, Emmanuel Okwi raia wa Uganda ndiyo mchezaji bora wa Ligi Kuu bara Agosti mwaka 2017.
Okwi amechaguliwa mchezaji bora na kuwashinda, Mohamed Issa wa Mtibwa Sugar pamoja na Boniface Maganga wa Mbao FC.
Ni baada ya kufanya vizuri katika mechi yao ya kwanza walipoifunga Ruvu Shooting mabao 7-0, yeye akipachika manne na kuondoka na mpira wa hat-trick.
Mbali na ushindi huo, ameweka historia ya kufunga hat-trick ya kwanza msimu huu pamoja na mchezaji bora wa kwanza wa msimu huu. Amepata kitita cha Sh1mil zawadi ambayo hutolewa kwa kila mchezaji wa mwezi anayetangazwa kwa ubora.
Wachezaji alioshindanishwa nao kwa upande wa Maganga, aliingia kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kufanya vizuri katika mechi yao ya ugenini walishinda kwa Kagera Sugar 1-0, ndiye alifunga.
Iko hivyo pia kwa Mohamed Issa ambaye alifunga bao pekee na kuipa ushindi timu yake iliposhinda kwa Stand United 1-0 Manungu, Morogoro.
Thursday, 14 September 2017
Home
Unlabelled
Okwi aanza kwa kishindo ligi kuu, abeba Tuzo ya mchezaji bora Agosti
Okwi aanza kwa kishindo ligi kuu, abeba Tuzo ya mchezaji bora Agosti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment