Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea ameugua ghafla na kupumzishwa katika zahanati ya Bunge.
Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema leo Alhamisi jioni kuwa mbunge huyo alikwenda katika zahanati hiyo baada ya kujisikia vibaya.
“Alijisikia kukosa nguvu akaenda katika zahanati hiyo, amepumzishwa na sasa hivi ndio anasema ni simu yake ya kwanza kuongea nayo tangu apumzishwe. Ndio kwanza amekaribia kumalizia dripu,” amesema Silinde.
Hata hivyo waandishi wa habari walipofika katika zahanati hiyo hawakuruhusiwa kumuona na badala yake wauguzi walisema amepumzika.
Daktari wa zahanati ya Bunge, Dk Noel Solomoni amethibitisha kupumzishwa kwa mbunge huyo tangu saa 10 jioni leo.
Hata hivyo, hakuwa tayari kueleza zaidi kama alifikishwa ama alikwenda mwenyewe katika zahanati hiyo iliyopo ndani ya Bunge.
Thursday, 14 September 2017
Home
Unlabelled
Dodoma: Saed Kubenea augua gafla, akimbizwa hospitali
Dodoma: Saed Kubenea augua gafla, akimbizwa hospitali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment