Ofisi ya Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo yavamiwa na watu wasiojulikana watoweka na kabati la kutunzia nyaraka na fedha. Watu wasiojulikana usiku wa kuamkia jana wamevamia na kufanya uharibifu katika Ofisi za Wanasheria wa Prime Attorneys
KIASI cha shilingi milioni tatu na laki saba, Hati za wateja tofautitofauti pamoja na nyaraka mbalimbali za ofisi ya mawakili ya Prime Attorney advocate zilizopo upanga jijini Dar es Salaam zaibwa na watu wasiojulikana wakati walipovamia ofisi hiyo majira ya saa tisa na nusu usiku.
Hayo yamesemwa na wakili, Asia Charles akizungumza kwa niaba ya Wakili Hudson Ndusyepo wakati akizungumza na Michuzi Blog leo amesema kuwa “Ni kweli Majambazi hao walifanikiwa kuvunja milango ya ghorofa ya kwanza na ya pili hawakuchukua kitu chochote na wakafanikiwa kupanda mpaka ghorofa ya tatu upande wa kushoto waliingia ofisi ya Mhasibu na kufanikiwa kuchukua kabati binafsi (Self) ambalo lilikuwa na Nyaraka za Ofisi, pesa shilingi milioni Tatu na laki saba pamoja na Nyaraka mbalimbali za Wateja".
Amesema kuwa Watu hao wamecheza zaidi na Vitasa vya Milango na kufanikiwa kufungua Milango na kuiba Kabati Binafsi (Self) walilokuwa wanalitaka.
Asia maesema kuwa Mlinzi alieleza kuwa walipofika katika ofisi hizo alijitahidi kuwazuia lakini wakamshinda kutokana na kumzidi nguvu pamoja na uwingi wao, pia mlizi amesema aliwaambia kuwa walimwambia asiongee kitu chochote na wakamuamlisha awapeleke wanakotaka na baadae baada ya kufika wakamziba mdomo na Plasta Nyeusi ili asiweze kupiga kelele.
"Tunasubiri Uchunguzi wa Polisi Ukamilike ndio tunaweza tukatoa taarifa kamili" Amesema Asia.
Wakili, Asia Charles akizungumza na Mwandishi wa Michuzi Blog jijini Dar es Salaam leo amesema kuwa Kiasi cha shilingi Milioni Tatu pamoja na Nyaraza za ofisi ya Prime Attorney advocate pamoja hati mbalimbali za wajeja wao zimeibwa na watu wasiojulikana walipovamia Ofisi hiyo Usiku wa Kuamkia leo Upanga jijini Dar es Salaam.
Tuesday, 12 September 2017
Home
Unlabelled
Ofisi ya wakila wa Manji yavamiwa na watu wasiojulikana
Ofisi ya wakila wa Manji yavamiwa na watu wasiojulikana
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Vat leaching gold processing method is the recently technology that practised in developing nations. In Tanzania vat leaching method w...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
No comments:
Post a Comment