Niyonzima na Liuzio washidwa kufanya mazoezi - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 12 September 2017

Niyonzima na Liuzio washidwa kufanya mazoezi

 
 Nyota wawili wa klabu  Simba SC, Haruna Niyonzima na Juma Liuzio wameshindwa kufanya mazoezi jioni ya Jana katika uwanja wa Uhuru kutokana na afya zao kutokuwa vizuri.

Wachezaji hao walifika uwanjani hapo kuwashuhudia wenzao wakifanya mazoezi lakini walishindwa kufanya mazoezi kutokana na kusumbuliwa na matatizo tofauti tofauti ya kiafya.

Daktari wa klabu ya Simba SC, Yasini Gembe Amesema kuwa Niyonzima anasumbuliwa na malaria wakati Liuzio akiwa na tatizo la mafindofindo ( tonses) lililompelekea spate homa na kumfanya kushindwa kufanya mazoezi.

Gembe Amesema pia kuwa nyota hao watakuwa wamepata nafuu kabla ya  mchezo wa unaofuata wa ligi kuu dhidi ya Mwadui FC utakaofanyika katika uwanja wa Uhuru jumapili ijayo.

"Niyonzima na Liuzio wameshindwa kufanya mazoezi jioni ya Jana kwa vile hawapio fiti ila tunategemea kabla ya mechi ya Mwadui FC watakuwa wamerudi uwanjani" alisema Gembe.

Mshambuliaji Emmanuel Okwi na beki Juuko Murshid ambao walikosekana katika mchezo uliopita dhidi ya Azam FC kutokana na kuchelewa kuripoti kambini wakitokea kwenye majukum ya timu ya Taifa ya Uganda ' The Cranes' walikuwepo kwenye mazoezi.

No comments:

Post a Comment

Popular