Mwanza :Kiwanda cha nyaya za umeme chateketea kwa moto - KULUNZI FIKRA

Tuesday, 26 September 2017

Mwanza :Kiwanda cha nyaya za umeme chateketea kwa moto

 
Kiwanda chote cha  Multi Cable Limited kilichopo  eneo la Kijereshi kata ya Igoma jijini Mwanza ,kimeteketea kwa  moto leo.

Kiwanda hicho kimeanza kuwaka saa nane mchana huku chanzo kikibainika ni kutokana na   hitilafu ya nguvu za umeme.

Kiwanda hicho cha Multi Cable Limited kinajihusisha na utengenezaji wa nyaya za umeme na bomba za kupitisha nyaya hizo.

Mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda hicho, anasema wao walishtukia moshi ukiwa unatokea  kwenye 'store'  wakagundua kwamba ni nyaya zimegusana kwenye paa na kusababisha moto huo.

No comments:

Post a Comment

Popular