Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kulitaka jeshi la polisi nchini kutokisaidia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema wamuache yeye na CHADEMA wapambane kukiondoa chama hicho madarakani kwani kimeshachoka
Msigwa amesema kitendo cha polisi juzi kummamata wakati akiwa kwenye majukumu yake ya kibunge kimemuudhi sana na kusema ni jukumu la Mbunge yoyote yule kuelimisha jamii, kuwapa habari wananchi pamoja na kuikosoa serikali.
"Mimi nilikuwa sifanyi uchochezi kazi ya Mbunge kuelimisha, kuhabarisha, kuikosoa, kuisimamia serikali na kuchochea maendeleo katika jimbo kwa hiyo kama Mbunge ninayo haki ya kuzungumzia Demokrasia na haki ya kuzungumzia mambo ya utawala bora, nina haki ya kuzungumzia haki za binadamu , kitendo cha polisi kunikamata juzi kimeniudhi sana hao polisi waniache mimi na chama changu tupambane na CCM, wasiisadie CCM kwani saizi imechoka ipo dhohofu yaani ipo taabani wanajaribu kuitetea CCM, wajitokeze CCM wenyewe wajibu hoja"alisema Msigwa
Msigwa aliendelea kusema kuwa yeye ni Mbunge ana haki ya kuikosoa serikali iliyopo madarakani hata kuichonganisha na wananchi ili wasiichangue tena mwaka 2020 anadai huo ndiyo wajibu wake kisiasa na ndiyo maana anakuwa mpinzani.
Tuesday, 26 September 2017
Home
Unlabelled
Mchungaji Peter Msigwa: Chama cha mapinduzi kimechoka
Mchungaji Peter Msigwa: Chama cha mapinduzi kimechoka
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...

No comments:
Post a Comment