Mbowe: Jumla ya Tsh 204M za matibabu ya Lissu zimechangwa na makundi mbalimbali. - KULUNZI FIKRA

Friday, 22 September 2017

Mbowe: Jumla ya Tsh 204M za matibabu ya Lissu zimechangwa na makundi mbalimbali.

 
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Salim Mwalimu :Leo tumeona tuje kwenu tuwaeleze yaliyomtokea Tundu Lissu toka siku ya kwanza hadi leo. Mwenyekiti Mbowe atatueleza.

●Freeman Mbowe "Nitazungumza kuwa taarifa rasmi kuhusu hali halisi ya Tundu Lissu."

●Freeman Mbowe:"Nianze na habari njema; Tundu Lissu anawasalimu sana. Nimeachana naye Nairobi jana mchana nikamwambia nitazungumza na Watanzania."

Freeman Mbowe "Akaniomba nimpelekee salamu zake kwamba Mungu anaendelea kumpigania na In Shaa Allah baada ya muda atarejea kwa mapenzi yake."

Freeman Mbowe"Shambulio lile halikuwa kwa Lissu peke yake, lilikuwa shambulio la Chama, kauli ya Haki, Ubinadamu na Watanzania kupitia Lisu."

Freeman Mbowe"Lissu amebeba majeraha mengi, maumivu makali kwa kauli zake za kulitetea Taifa lake, kuwatetea Watanzania wenzake na kudai haki."

Freeman Mbowe: "Kumekuwa na kauli nyingi sana, ndugu zangu Watanzania pamoja na kiu ya kupata habari hili sio jambo la kuuzia magazeti."

Freeman Mbowe: "Sio jambo la kujipa umashuhuri kwenye mitandao ya kijamii kwa kuandika kauli zisizo rasmi na sio thabiti."

Freeman Mbowe "Jambo hili limesababisha usumbufu mkubwa sana sio kwa familia ya Lissu hata kwa wanachama na madaktari wanaomhudumia Nairobi."

Freeman Mbowe: "Tundu Lissu yupo chini ya ulinzi mkali sana saa 24 nje na ndani... hatuwezi kufanya uzembe tena"

Freeman Mbowe: "Wameleta malalamiko namna vyombo vya habari vya Tanzania vimekuwa vinapotosha taarifa mbalimbali za ugonjwa au madhila ya Lissu." -

Freeman Mbowe: "Mashine yetu 'Lissu' itarudi barabarani salama kabisa ikiwa timamu, nataka niwaeleze ufahamu wake uko vizuri 100%"

Freeman Mbowe Wapo wengine wamefika Hospitali wamemuona na wengine hawakumuoa, wanatoka nje ama wanaongeza chumvi au wanaeleza mambo yasiyo kweli."

Freeman Mbowe: "Sitomtaja mmoja baada ya mwingine ila itoshe kuwaomba Waandishi, viongozi wenzangu tuungane kuwa taarifa za ndani ni siri ya mgonjwa"

Freeman Mbowe "Taarifa kwamba Lissu leo amekaa, Lissu leo amekula hizi ni uongo ambao unaleta mtafaruku na hofu kubwa kwa Watanzania."

Freeman Mbowe :"Lissu hakukata kauli mpaka anaingia theatre, pamoja na majeraha yote hajawahi kukata kauli" -

"Niwaombe rasmi kwa niaba ya Chama, madaktari, familia kuwaomba sana Watanzania, kauli zisizo rasmi zisipewe nafasi." Mbowe

."Nisistize kwamba taarifa rasmi za chama zitatolewa na mimi mwenyewe nikiwa ama Dar es Salaam au Nairobi." Mbowe.

"Hali ya mgonjwa, Lissu alifikishwa Nairobi usiku saa sana, hali yake ilikuwa ngumu sana. Madaktari walitupokea na kuanza kumhudumia." Mbowe

"Madaktari wanasema ni miujiza kutoka salama bila kukatwakatwa kwa risasi ktk shambulio kama la Lissu"-MBOWE

"Lissu anatibiwa na kundi kubwa la madaktari na ningependa niwatambue waingie kwenye rekodi kwa kazi ya ziada kuokoa maisha ya Lissu." Mbowe

"Kabla ya madaktari wa Nairobi, niwashukuru madaktari wa Hospitali ya Dodoma. Kama wasingefanya wajibu wao wa msingi tusingesafiri na Lissu"

"Katika mazingira magumu walifanya kazi ngumu kwa haraka na presha kubwa sana kuweza kuzuia damu kutokana na risasi na majeraha makubwa."Mbowe

"Kazi kubwa iliyofanywa na madaktari wa dodoma tusiipuuze, ilituwezesha kufika Nairobi akiwa hai. Ilikuwa ni miujiza kila mmoja alishangaa."Mbowe.

"Madaktari wa Kenya walishangaa imekuwaje huyu mtu kwa shambulio na majeraha haya bado anapumua." Mbowe.

"Mipango ya Mungu ni mikubwa kabisa kuliko ya wahalifu. Tunashukuru kwa walichokifanya madaktari kumzindua." Mbowe.

"Taarifa ya madaktari kuhusu hali ya Lissu imetolewa ni siri na itoshe tu kuwapa kwa upande huo." Mbowe.

"Niseme tu kwamba hali ya Lissu kwa sasa imeimarika, hofu ya uhai wake kupotea madaktari wanasema haipo tena labla kwa jambo jingine." Mbowe

"Matibabu yanaendelea na nizungumze kuhusu mipango ya kumpeleka nje ya nchi zaidi kwa ajili ya matibabu." Mbowe.

"Zimezungumziwa na watu wengi, zingine za kupotosha na nyingine za kuvuruga tu." Mbowe.

"Nizielezee kidogo zipo juhudi nyingi za viongozi wa chama wapenzi wa chama na wanachama walio nje ya nchi na watanzania" Mbowe.

"Kuna presha ya kumpeleka nchi tofauti sita; wapo waliotaka apelekwe A. Kusini, wengine India, Ubelgiji, Ujerumani, UK na USA" Mbowe

"Makundi yote yalifanya kazi hii kwa nia njema bahati mbaya vyombo vya habari vimekuwa vikiandika taarifa zisizothibitishwa." Mbowe.

"September 20 tulifanya kikao kikubwa cha kutathmini hali ya mgonjwa kikiongozwa na mimi kujua hali yake" Mbowe.

"Kama kiongozi wa Chama nadiriki kusema kwamba mshukiwa namba moja wa shambulio la Lissu ni vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi hii" Mbowe.

"Hilo nalisema bila kumung'unya maneno, viashiria vyote vya tukio lile tangu linatokea kauli na kusita kwa viongozi na kauli za kujiosha."Mbowe

"Ni nani katika vyombo vya ulinzi na usalama, simjui lakini ni vigumu sana kusema tukio la ujambazi, hakuna ujambazi pale." Mbowe.

"Hadi sisi kudai vyombo huru vya kiuchunguzi ni kutokana na madhila mbalimbali tueyapata tukaona vyombo vya ndani havina msaada." Mbowe.

"Baada ya Uchaguzi wa 2015, aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Geita, Alphonce Mawazo alishambuliwa mchana kweupe na watu wanaojulikana." Mbowe.

"Wanasema waliomshambulia hawajulikani, sisi tunasema waliomshambulia Mawazo wanajulikana." Mbowe.

"Polisi walisema wanachunguza, hawakuchunguza. Mwaka wa pili sasa unakwisha Mawazo amesahaulika." Mbowe.

"Ben Saanane amepotea msaidizi wangu unakwenda mwaka wa pili sasa, tumepiga kelele ndani na nje ya Bunge, vyombo vya habari hakuna kitu."

"Jaji Mkuu anasema uchunguzi utafanyika ndani, tunamwambia asubiri ushahidi Mahakamani, uchunguzi ni mambo ya Polisi." Mbowe.

"Tunapoomba msaada wa kiuchunguzi ni kwa sababu hatuna imani na mamlaka za uchunguzi wa ndani." Mbowe.

"Watu wetu wamepotea, watu wetu wameuawa, wanapigwa risasi mchana kweupe na hakuna hatua ya maana inayofanyika." Mbowe.

"Hatuna imani kama safari hii kutakuwa na tofauti. Ndio sababu ya msingi ya sisi kutaka msaada kutoka nje." Mbowe.

Mhe. Freeman Mbowe Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa anasema;

=>Siwezi kusema kwamba kuna mtu yeyote upande wa bunge hakutupa ushirikiano

=>Tulishirikiana nao Tukapata ndege kutoka jet

=>Hata kama ndege imelipiwa na CCM, ukweli ni kwamba fedha zote zimelipwa na CHADEMA.

=>Waziri anasema serikali inaweza kumpeleka Lissu popote duniani kumtibu hawakumbuki pale Dodoma walivyoniambia, wamuogope Mungu.

Nitaeleza hali ya michango na gharama ya matibabu.

=>Hawataweza kuichafua CHADEMA.

=>Kuna wanaosema CHADEMA ndio wamehusika wanagombania vyeo, huo ni upumbavu.

=>Tulikubaliana kila mbunge wa CHADEMA achange laki 5 na baadae wabunge wakachanga tena laki5.

Wabunge CHADEMA=48,465,000

Wananchi=24,200,000

Wananchi CRADB=52,0000,000

Wabunge=43,000,000

Jumla=147,667,000

Fedha zote zimelipwa isipokuwa 43,000,000 ya wabunge

=>Wabunge walikubaliana wabunge wenyewe wachange.

=>Walichanga 43,000,000. Spika alinipigia simu na katibu wa bunge.

=>Niliwaambia akaunti imetolewa wekeni humo.

=>Spika akanipigia tena na kusema hawawezi kuweka kwenye akaunti ya chama, tupeni uthibitisho wa matibabu na akaunti ya hospitali.

=>Bado fedha hizo mpaka sasa hazijawekwa.

=>Ni bora masikini anayetoa kwa moyo kuliko tajiri anayetoa kwa masimango

Fedha zilizochangwa kupitia gofundme dola 20,329 kama milioni arobaini na kitu.

Baada ya makato, pesa inayoletwa kwenye chama dola 20,387

Jumla fedha zote ni milioni 204.

=>Niwashukuru TLS wametoa dola elfu 9 moja kwa moja hospitali.

=>Kundi la watanzania wanaoishi Kenya walikuja hospitali kutoa damu.

=>Ingekuwa hawakutoa damu Lissu asingekuwa hai.

=>Damu iliyomponya Lissu si ya wanachadema ni ya watu ambao hatuwajui.

=>Nimesikitika sana, vongozi wetu waliwasisitiza watu wetu wachange damu zikawasaidie watu wengine,Polisi wakawakamata

=>Kundi la watu 18 walienda Temeke hospitali kuchangia damu wakawekwa ndani siku mbili.

=>Polisi wanawazuia watu kufanya maombi.

=>Hili jambo limetuumiza sana watanzania,

=>Jana mh Jaji mkuu alisema vyombo vya ndani havijashindwa kufanya uchunguzi.

=>Mimi kama mwenyekiti wa chama nasema suspect namba moja ni vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali.

=>Baada ya uchaguzi wa 2015, mwenyekiti wa mkoa wa Geita aliuawa, polisi hawakufanya uchunguzi mpaka leo.

Msaidizi wangu Ben Saanane naye amepotea.

=>Ruhusuni vyombo vya ulinzi na usalama kutoka nje.

=>Chief Justice hahusiki na uchunguzi akumbuke tunamuheshimu sana.

=>Hatuna imani na vyombo vya ndani.

=>Nimalizie na gharama za matibabu.

=>Hii ni ripoti ya matibabu ya kila kitu kuhusu vipimo na matibabu aliypopata Lissu.

=>Mpaka juzi tare 20/09/2017. Milioni 6 za Kenya. Leo gharama zimeshafikia 7,400,000 sawa na 162,800,000 za kitanzania.

=>Tunaomba watanzania waendelee kuchanga.

Spika alinipa masharti haya ili serikali igharamie matibabu ya Lissu;

Apelekwe India.

Niandike barua

Nipeleke taarifa ya matibabu.Sikufanya

Jana Ummy anasema familia ipeleke maombi.

Huyu ni mbunge .

Familia ikiamua sina kipingamizi

Nawashukuru makundi yote yaliyojitokeza kufanya maombi.

=>Nawasihi waandishi msichukue habari za udaku na kuzitoa kwa wananchi, acheni zinawaumiza familia yake.

=>Tunawashukuru sana kwa namna ambavyo mmekuwa mstari wa mbele kuripoti usiku na mchana.

=>Nawashukurini sana kwa kunisikiliza.

=>Hao ambao wanasema wako tayari, tutawasikiliza wako tayari kiasi gani. utayari wao hauna mashaka wala malengo mabaya.

Swali: Lisu anaamini ni nani aliyemshambulia?

Majibu: Tumeona kauli nyingi zinazosemekena zimetoka kwa LIssu.

Siku kauli rasmi ikitoka kutoka vyanzo vyetu

Kauli ikitoka nitawaambia. Heshimuni kauli.

Swali: CHADEMA mlisema mnamsapoti Jubilee na CCM nao hivyo hivyo NASA. Hamuoni NASA wakishinda ulinzi wake utakuwa mashakani?

Majibu: Wajibu wa ulinzi ni jukumu la serikali. Ulinzi tuliomba kutoka utawala wa hospitali. Na ikiingia hata serikali nyingine ulinzi wa Lissu utakuwa palepale.

Swali: Masharti gani mnataka serikali iyatimize?

Majibu: Tulifanya kikao na ummy tarehe 7/09/2017. Alisema serikali haitibu mtu popote isipokuwa India. Jana alisema serikali ipo tayari kumtibu popote ikiwa serikali. Kama familia ikiridhia hatuwezi kukataa

=>Misaada yenye nia njema tutaipokea, misaada yenye nia kiitikadi tutaikataa.

=>Vyombo vyetu vina uwezo. Ila kwa masuala ya upinzani vinatiwa ubutu.

=>Watu wa Scotland Yard, FBI na waisrael wako tayari

Swali: Kwanini chama hakijafungua kesi?

Majibu: Kesi unafungua kwa nani na anayechunguza ni nani? Na anaye-investigate ni nani? Ni kama kesi ya nyani unampelekea tumbili.

Hatuna tatizo la kufungua kesi. Priority yetu ya kwanza kuokoa maisha ya Mh Lissu.

Swali: Kwanini dereva hajatokea kutoa ushirikiano kwa polisi.

Majibu: Dereva alipitia madharuba makubwa ambapo alihitajika kupata counseling.

Dereva katika mazingira yaliyokuwepo. Huyu dereva amekuwa na Lissu miaka mingi na ni ndugu yake. Ni mtu wake wa karibu. Watu wana tabia ya kuwashambulia watu na wakiona hawakuwamaliza vizuri, wanawarudia.

Hawa watu hawakuwa mtu mmoja, ilikuwa ni kundi la watu.

Dereva wa Lissu akimaliza matibabu atasema na Lissu mwenyewe atasema.

Ni risasi ngapi zilizompata mh Lissu.

Risasi zilikuwa nyingi. Kuhusu suala la risasi ngapi atalisemea mwenyewe.

No comments:

Post a Comment

Popular