Madiwani wawili wa Chadema Emmanuel Mwalupasa na Jailo Mwandute katika Halmashauri ya Mji wa Tunduma wilayani Momba wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kwa makosa tofauti ya jinai.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange amesema Mwalupasa ambaye ni diwani wa Mpande anatuhumiwa kufunga ofisi ya mtendaji kata kwa siku tatu mfululizo.
Kuhusu diwani Mwandute wa Kata ya Katete, amesema anatuhumiwa kwa wizi wa zaidi ya Sh10 milioni ambazo ni kwa ajili ya maendeleo ya kata hiyo.
Kamanda Nyange amesema madiwani hao walikamatwa jana Alhamisi jioni na kufikishwa kituo kikuu cha polisi mjini Tunduma ambako wanaendelea kushikiliwa.
Amesema wanaendelea na uchunguzi kuhusu tuhuma zinazowakabili madiwani hao.
Friday, 29 September 2017
Home
Unlabelled
Madiwani wawili wa chadema washikiliwa na polisi
Madiwani wawili wa chadema washikiliwa na polisi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment