Maalim Seif: Sio aibu kupata msaada kutoka nje kuchunguza shambulio la Tundu Lissu - KULUNZI FIKRA

Wednesday, 27 September 2017

Maalim Seif: Sio aibu kupata msaada kutoka nje kuchunguza shambulio la Tundu Lissu

  Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema si aibu kwa nchi kupata msaada kutoka nje kuchunguza tukio la kushambuliwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Aidha, amesema anaunga mkono kauli ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, kwamba vyombo vya ndani vinaweza kufanya hivyo na kuongeza kuwa ni muhimu wananchi waambiwe kinachoendelea.

"Nadhani ni vizuri wananchi wakaona matokeo yake kwa sababu hatujaambiwa hasa nini kinaendelea, si vibaya kupata msaada toka nje, hiki ndicho kinatokea duniani huko", amesema Maalim Seif wakati akihojiwa na Radio Deustche Welle (DW) ya Ujerumani leo.
    

No comments:

Post a Comment

Popular