Mbunge wa Ubungo (Chadema) Saed Kubenea amesema aliugua ghafla akiwa njiani kuelekea katika Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Amesema aliitikia wito wa Spika Job Ndugai ambaye Jumanne wiki hii alimpeleka mbele ya kamati hiyo.
Spika alisema Kubenea anamtuhumu kwenye mitandao ya kijamii kuwa amesema uongo kuhusu idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.
Kubenea amesema alitakiwa kuripoti mbele ya kamati saa 7:30 mchana lakini alipokwenda aliambiwa kuna shughuli za Bunge zimeingiliana hivyo arejee saa 9:30.
Mbunge huyo amesema hakuweza kurejea mbele ya kamati baada ya kuugua ghafla.
“Nilishaenda kwa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, wakati ninakwenda kwa Kamati ya Maadili nikapata tatizo,” amesema Kubenea.
Awali, Katibu wa Wabunge wa Chadema, David Silinde alisema Kubenea alikwenda kwenye zahanati ya Bunge baada ya kujihisi vibaya.
“Alijisikia kukosa nguvu akaenda zahanati, amepumzishwa na sasa anasema ni simu yake ya kwanza kuongea nayo tangu apumzishwe. Ndiyo amekaribia kumaliza dripu,” alisema Silinde.
Daktari wa zahanati ya Bunge, Noel Solomoni alithibitisha kupumzishwa kwa mbunge huyo tangu saa kumi jioni.
Thursday, 14 September 2017
Home
Unlabelled
Kubenea azungumzia yaliyomsibu
Kubenea azungumzia yaliyomsibu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Vat leaching gold processing method is the recently technology that practised in developing nations. In Tanzania vat leaching method w...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
No comments:
Post a Comment