KIKOSI cha Simba, kinaendelea vema na mazoezi yake pale Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, lakini kocha Joseph Omog amesikia kelele za mashabiki kuhusu Jonas Mkude na kuamua kuanika siri za nahodha huyo wa zamani.
Omog anayeuguza jeraha kichwani baada ya kupigwa kichwa kwa bahati mbaya na straika Emmanuel Okwi kwenye mazoezi ya timu hiyo juzi, alisema kikosi cha Simba kina wachezaji wengi wazuri ila eneo la kiungo mkabaji ni pasua kichwa.
Mcameroon huyo alisema nafasi hiyo inayochezwa na Mkude na James Kotei humpa kazi ya kuchagua wa kumwanzisha kwa vile wote wapo vizuri mno.
Alisema watu wanaweza kudhani hapendi kumtumia Mkude labda ana tatizo naye, ila ukweli ni kwamba hupata wakati mgumu kuamua nani acheze kwa sababu wote ni wazuri japo wanazidiana vitu vichache.
“Kwa uwezo wa Mkude huwezi kumuacha mchezaji kama huyo, watu watulie watamuona tu uwanjani,” alisema.
Lakini juzi Jumanne na jana Jumatano, kulunzifikra blog limeshuhudia Mkude akifanya mazoezi na wachezaji wa kikosi cha kwanza kuashiria kwamba huenda Jumapili akawepo uwanjani Simba itakapoikabili Mwadui FC kwenye Uwanja wa Uhuru.
Hakuna bifu
Mkude na nahodha wa sasa wa Simba, Method Mwanjali, hutupiana maneno kiasi mtu kama hujui unaweza kudhani wana bifu, lakini Mzimbabwe amefichua ndio maisha yao kambini.
“Mkude ana masihara na anapenda kunitania kama tuna ugomvi vile, lakini ndivyo tulivyozoeana na hakuna shida yoyote baina yenu,” alisema Mwanjali baada ya Mwanaspoti kuwashuhudia wakirushiana maneno.
OKWI AMPASUA OMOG
Katika mazoezi ya juzi, Omog alipasuka usoni alipogongana na Okwi aliyekuwa akitaka kuupiga mpira kwa kichwa kuunganisha krosi ya Ally Shomary.
Kocha huyo alilazimika kuwekwa plasta katika jeraha lililovuja damu, Okwi yeye hakuumia.
Thursday, 14 September 2017
Home
Unlabelled
Kocha mkuu wa klabu ya Simba SC Omog amuanika Mkude
Kocha mkuu wa klabu ya Simba SC Omog amuanika Mkude
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri nchini (KKKT), Askofu Dkt Fredrick Shoo amefunguka na kusema kuwa kama taifa linahitaji maendeleo...
-
Mbunge wa Jimbo la Temeke (CUF), Mhe Abdallah Mtolea amefunguka na kuweka wazi kuwa mgogoro uliopo ndani ya Chama chake umekuwa ukiathir...
-
Vat leaching gold processing method is the recently technology that practised in developing nations. In Tanzania vat leaching method w...
-
Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto kubwa katika uhitaji wa uzoefu katika nafasi za kazi(work Experience) kwa vijana wa Tanzania. ...
No comments:
Post a Comment