Klabu ya Simba SC yabanwa mbavu Tabora - KULUNZI FIKRA

Monday, 25 September 2017

Klabu ya Simba SC yabanwa mbavu Tabora

 
Wekundu wa Msimbazi Timu ya Simba SC imeshindwa kufurukuta mbele ya timu ya Milambo FC katika mchezo wake wa kirafiki uliopigwa jana katika dimba la Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora ambapo imelazimishwa suluhu.

Katika mechi hiyo iliyochezwa huku mashabiki lukuki wakifurika katika uwanja huo, Simba ilishindwa kuwafurahisha mashabiki wake kwa kuonekana imezidiwa nguvu na timu hiyo ya Milambo inashiriki ligi daraja la pili Tanzania Bara.

Simba ikiwa imewachezesha wachezaji wake nyota John Bocco, Haruna Niyonzima, Mohamed Ibrahim,Laudit Mavugo, James Kotei na wengineo lakini walionekana kuzidiwa ufundi na wakongwe hao wa soka la Bongo ambao wamepotea ligi kuu kwa miongo kadhaa.

Msemaji wa timu ya Simba, Hajji Manara akizungumzia mchezo huo amekubali kiwango kilichooneshwa na Milambo na kubainisha kuwa jicho lao limegundua Milambo kusheheni wachezaji wenye uwezo wa kutosha kucheza ligi kuu .

No comments:

Post a Comment

Popular