Kesi ya meno ya tembo inayomkabili Yusuf Ali,maarufu mpemba wa Magufuli sasa kupelekwa mahakama ya mafisadi - KULUNZI FIKRA

Tuesday 5 September 2017

Kesi ya meno ya tembo inayomkabili Yusuf Ali,maarufu mpemba wa Magufuli sasa kupelekwa mahakama ya mafisadi

 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa, hati ya mashtaka ya kesi ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo dhidi ya mfanyabiashara Yusuf Alli maarufu kama mpemba wa Magufuli’ inatarajiwa kupelekwa Mahakama ya mafisadi.

Hayo yameelezwa na wakili wa serikali, Elia Athanas mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba kesi hiyo ilipokuja kwa kutajwa. "Mheshimwa, jalada la kesi hii limekamilika, hivyo naomba muda ili wapeleke hati ya mashtaka Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi 'Mahakama ya Mafisadi'.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi September 19/2017.

Yusuf anashtakiwa pamoja na Charles Mrutu, mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa, mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima, mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo, dereva na Pius Kulagwa, wanakabiliwa na mashitaka manne ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh.milioni 785.6.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, mwaka huu wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara, walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za serikali ambazo ni

vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh milioni 392.8 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Watuhumiwa hao wakiwa katika viunga vya Mahakama ya Kisutu,mapema leo kwenye kesi yao ya kudaiwa kujihusisha na biashara ya meno ya tembo,ambayo kwa sasa inatarajiwa kupelekwa Mahakama ya mafisadi.

No comments:

Post a Comment

Popular