Kasulu Kigoma: mtu mmoja auawa kwa kuchomwa moto huku nyumba 7 zikiteketezwa kwa moto. - KULUNZI FIKRA

Tuesday 5 September 2017

Kasulu Kigoma: mtu mmoja auawa kwa kuchomwa moto huku nyumba 7 zikiteketezwa kwa moto.

 

Mtu mmoja anayejulikana kwa jina la Emmanuel Songoye, ameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi katika kijiji cha Kabanga, wilayani Kasulu mkoani Kigoma.

Katika tukio ambalo pia wameteketeza kwa moto nyumba saba, magari mawili, pikipiki nne na mali za familia za watu sita ambao wanamtuhumu kufanya mauaji ya watu Kijijini hapo kwa njia ya mbalimbali ikiwa ni pamoja na ushirikina ili watajirike.

Naibu Kamishna wa polisi Kigoma Ferdinand Mtui, amesema zaidi ya watu hamsini wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo huku Kaimu mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Marco Gaguti ambaye pia ni mkuu wa  wilaya ya Buhigwe akitoa wito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.

No comments:

Post a Comment

Popular