Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, anaungana na Rais Magufuli, viongozi wengine na wananchi, katika kumuombea Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu aliyepingwa risasi.
Ameyasema hayo hii leo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akisoma hotuba ya kughailisha Bunge, ambapo amesema kuwa anamuombea Tundu Lissu ili aweze kupona na kurejea katika hali yake ya kawaida na kwenye shughuli zake za jamii.
"Naungana na Mh, Rais Dkt.John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Spika wa Bunge Job Ndugai, Wabunge na Wananchi mbalimbali, kumpa pole kwa majeraha na maumivu makubwa anayoyapata, na tunamuombea apone haraka na kurejea kwa familia yake".
Aidha, Majaliwa amesema anamuombea mbunge huyo apone haraka zaidi ili aweze kurejea bungeni kuendelea na majukumu yake ya kila siku ya kuwatetea na kuwasaidia wananchi wanaohitaji huduma yake.
Hata hivyo, Majaliwa ameghailisha shughuli za Bunge kwa mujibu wa sheria mpaka ifikapo Novemba 7 mwaka 2017 litakapoanza vikao vyake tena kwa mara nyingine.
Friday, 15 September 2017
Home
Unlabelled
Dodoma: Waziri mkuu aungana na Rais Magufuli kumuombea Tundu Lissu
Dodoma: Waziri mkuu aungana na Rais Magufuli kumuombea Tundu Lissu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment