Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kutoa kauli yake baada ya serikali kusema ipo tayari kulipia gharama za matibabu ya Tundu Lissu popote duniani na kusema huo ni utani wa serikali ya awamu ya tano.
Mbunge Msigwa ametoa kauli hiyo baada ya masaa kadhaa kupita toka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kusema kuwa serikali ipo tayari kulipia gharama za matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu popote duniani baada ya kupata maombi kutoka kwa familia ya Tundu Lissu na kama ripoti ya madaktari itaonyesha kuna ulazima kiongozi huyo kupatiwa matibabu zaidi basi serikali itasimamia jambo hilo.
Kutokana na kauli hiyo Msigwa amedai huo ni utani wa serikali "Huu ni utani wa serikali ya awamu ya tano" alisema Peter Msigwa
Mbali na hilo Mbunge Peter Msigwa jana alisema kuwa wao wanatambua thamani na umuhimu wa Tundu Lissu na kusema kuwa wapo tayari kuuza vitu vyao mbalimbali ili kuhakikisha kuwa kiongozi huyo anapata matibabu na kurejea nchini akiwa salama.
Nae Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alikuwa na haya ya kusema
Kwa ufupi;
Asema nashangazwa sana na taarifa alizotoa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ya kwamba familia ya Lissu iandike barua kama wanahitaji matibabu na kwamba serikali ipo teyari kumtibu Mhe. Lissu mahali popote duniani.
Amemtaka Waziri huyo aache uongo na upotoshaji serikali haipo teyari kumtibu Lissu mahali popote Duniani ndio maana Spika kwa Kinywa chake alikataa ana akasisitiza kwamba wao wasingeweza kumtibu Lissu katika hospitali ya Nairobi ambapo sisi tuliamini kuwa kulikuwa na vifaa vya kuweza kuokoa uhai wake.
Pia amesema hakuna utaratibu wa kibunge ambapo mbunge anapokuwa mgonjwa kwamba familia yake ndio inaandika barua na kuelezea bunge kuwa huyu ni mbunge na anahitaji msaada wa kibunge. Bunge lina Katibu na Spika, Spika alikuwepo wakati Lissu anasafirisha anajua Lissu alipo lakini hajachua utaratibu wowote.
Amesema leo ni siku ya 14 lakini si Spika wa naibu wake wala Katibu wa mtu yeyote kutoka katika sekretariet ya bunge aliyewahi kurusha mguu kuja kujua anaendeleaje
Nae Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni na Mbuge wa Hai, Mhe. Freeman Mbowe akihojiwa na Sauti ya America jioni hii, alikuwa na haya ya kusema;
Kiongozi wa kambi rasmi ya upunzani bungeni na Mbuge wa hai Freeman Mbowe amekosoa vikali kauli ya serikali kuhusu utayari wa serikali kugharimia matibabu ya Lissu popote duniani.
Mbowe akihojiwa na Sauti ya America Washington, amekaririwa akiilamuu serikali kwamba imekaa kimya tangu jaribio la kumuua Tundu Lissu mpaka leo takribani wiki 2. Amenda mbali zaidi kwa kuhoji iweje serikali isubiri maombi kutoka familia ya Lissu ikiwa utaratibu wa matibabu ya Mbunge ndani na nje ya nchi yanashughulikiwa na bunge moja kwa moja kupitia kamati za bunge na kwamba hakuna mbunge aliewahi kupitia utaratibu huo.
Thursday, 21 September 2017
Home
Unlabelled
Baada ya serikali kusema ipo tayari kulipia matibabu ya Lissu; Peter Msigwa, Godbless Lema na Mbowe wakosoa kauli hiyo
Baada ya serikali kusema ipo tayari kulipia matibabu ya Lissu; Peter Msigwa, Godbless Lema na Mbowe wakosoa kauli hiyo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Tanzania’s Tunduru district is a major producer of gem-quality sapphire and ruby, along with exotic gems such as alexandrite and tsavor...
-
Moto mkubwa umelipuka na kuunguza soko la wafanyabiashara wadogo wadogo (machinga) katika eneo la Mbagala Rangi Tatu – Dar, asubuhi hii M...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...

No comments:
Post a Comment