Hatimaye wanachama 15 kati ya 51 wanaokabiliwa na shtaka la kosa kusanyiko lisilo halali katika mahakama ya wilaya ya chato mkoani Geita wameachiwa kwa dhamana Jana
Hili ni kundi la pili kuachiwa kwa dhamana yangu walipotimiza masharti julai 26, lakini wakaendelea kusota mahabusu ya gereza la Biharamulo mkoani Kagera kutokana na kukosekana kwa usafiri wa kuwafikisha mahakamani kukamilisha mchakato wa kuachiwa.
Kundi la kwanza la wanachama 14 liliachiwa Agosti 14 na hivyo kufanya waliopata dhamana kufikia 29 hadi Jana.
Wanachama hao wamekuwa wakitoka kwa mafungu ambapo fungi la kwanza lilitoka Agosti 14 mwaka huu kwa viongozi na wanachama 14 kupewa dhamana ambapo Jana wengine 15 wametoka na kufanya idadi yao kufikia 29.
Hakimu mkazi wa wilaya ya Chato, Jovith Kato amesema kuwa kundi lingine la watu 12 litaachiwa kwa dhamana kesho ( leo) Agosti 23 huku like la mwisho la watu 10 likiwa kesho kutwa
"Mahakama inalazimika kuwaachia kwa mafungu washtakiwa kutokana na wingi wao na mahitaji ya kupitia barua za wadhamini wawili kwa kila mshtakiwa",amesema .
Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani julai 10 na kunyimwa dhamana baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha hati ya zuio la dhamana.
Hata hivyo,Hakimu Kato alitupilia mbali zuio hilo julai 26, baada ya kukabiliana na hoja za wakili wa utetezi, Siwale Yisombi kuwa kifungu cha sheria kilichotumika kuweka zuio hakikuwa sahihi
Tuesday, 22 August 2017
Home
Unlabelled
Wanachama chadema waachiwa guru kwa mafungu
Wanachama chadema waachiwa guru kwa mafungu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
No comments:
Post a Comment