Akiwa katika ibada ya misa parokia Ya Sinza leo tarehe 13/08/2017, mwenyekiti wa bodi ya Parole nchini Ndg Augutino Mrema, ameshuhudia kuponywa kansa ya mapafu iliyomsumbua kwa muda mrefu.
Mrema akiyashuhudia hayo mbele ya Camera za ITV, alisema kuwa, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete alimsaidia sana wakati wa uongozi wake kwa matibabu. Alimpa msaada wa mara kadhaa kwenda kwenye matibabu India bila mafanikio.
Ndipo mwaka jana, Mrema akaonana na Paroko wa parokia ya sinza kuomba afanyiwe appointment na Kadinali Pengo. Alikwenda kwa Pengo na akaombewa. Paroko pia alimwombea mara kwa mara. Pia Mrema amesema aliomba pia waumini wote wa Sinza waendelee kumwombea.
Kutokana na Juhudi za juu za kuomba, Mrema alirudi tena hosipital mwaka huu na kukuta kansa ya mapafu iliyomsumbua muda mrefu haipo tena. Amesema alikua amekata tamaa na maisha ila sasa Yesu amemponya kabisa. Yu mzima.
Mrema pia ameongezea kwa kusema, Wapinzani wake kule Vunjo walitumia ugonjwa wake kama mtaji wa kampeni na kumwita marehemu mtarajiwa, na hatimaye wakafanikiwa kumnyang'anya jimbo lile.
Aliendelea kusema kuwa, Pamoja na ugonjwa wake, Rais JPM alipopita kwa kampeni Vunjo, aliwaomba wananchi wampigie Mrema kura. Pia amesema Rais aliahidi kumpa kazi hata kama akiwa mgonjwa. Ndiyo maana sasa ni Mwkt wa bodi ya parole.
Mrema aliyazungumza mengi huku akimwaga sifa tele kwa Rais JPM kuwa, ni Rais mwenye hofu ya Mungu na kwamba, mara kadhaa amekua akiwaasa watanzania wamtangulize Mungu mbele kwa kila jambo.
Mrema alimalizia kwa yeye, familia na jumuiya yake kutoa zawadi kwa parokia kama shukrani ya kuponywa ugonjwa hatari na sugu wa kansa ya mapafu.

No comments:
Post a Comment