Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, linaomba radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017.
Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga FC za Dar es salaam kwenye Uwanja wa Taifa jijini. Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao hiyo.
Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale, TFF hatujapokea vizuri mwonekano wenye makosa kwenye Ngao hiyo ya Jamii kama ambavyo wadau hawajapokea vema suala hili.
Kutokana na makosa hayo, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, tayari amechukua hatua za kinidhamu kwa watumishi waliohusika kadhalika kuwasiliana na uongozi wa Simba SC kuirejesha Ngao hiyo ili kufanyiwa marekebisho yatakayobaki kwenye Kumbukumbu sahihi.
Hatutegemei tukio kama hili kujirudia tena.
Thursday, 24 August 2017
Home
Unlabelled
Tff yaomba radhi kwa makosa ya maandishi kuhusu Ngao ya jamii
Tff yaomba radhi kwa makosa ya maandishi kuhusu Ngao ya jamii
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Popular
-
THIS ANNOUNCEMENT CONTAINS INSIDE INFORMATION Acacia Mining plc (“Acacia” or the “Company” or the “Group”) Management Changes Ac...
-
Spika wa zamani, Pius Msekwa amesema Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu hakuwa analazimika kuandika barua kwa Spika wa Bunge...
-
Wakati leo hii Rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta akiapishwa, Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Kikwete ametoa sababu kushin...
-
Ofisi ya Spika wa Bunge imesema, mpaka sasa haijapokea barua toka kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia Chama cha...
-
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetekeleza agizo la Rais John Magufuli kwa kumpatia ulinzi Ana-Joyce Francis, mjane mwenye watoto sita,...
No comments:
Post a Comment