Mwanafunzi apeta ubunge Kenya - KULUNZI FIKRA

Thursday, 10 August 2017

Mwanafunzi apeta ubunge Kenya



 Aliyekuwa mgombea wa ubunge Igembe kusini nchini kenya,John Mwirigi  (24) ameshinda nafasi hiyo baada ya matokeo kutangazwa na Tume guru ya uchaguzi na mipaka ( IEBC).
Mwirigi ambaye anatajwa kuwa mbunge mwenye umri mdogo kuwahi kutokea aliwashangaza wengi katika kampeni zake ambapo alikuwa akitumia baiskeli na bodaboda.
Mwirigi ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya elimu katika chuo cha Mount Kenya alikiuwa mgombea  binafsi, hakuwahi kuwa na matangazo kwa kile kilichodaiwa kukosa pesa za kufanya kazi hiyo.
Katika matokeo hayo ,Mwigiri  pia alipata kura 18,867 huku mgombea wa jubilee, Rufus Miriti alipata kura 15,411

No comments:

Post a Comment

Popular